UKOO WA URASSA.

– Urassa ni ukoo mkubwa wa kichagga na mashuhuri unaopatikana upande wa magharibi sana na mashariki sana ya Uchagga, Kilimanjaro. Hata hivyo ukoo wa Urassa pia unapatikana kwa kiasi maeneo ya katikati ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo uliotoa watu mbalimbali mashuhuri wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali za maisha katika siasa, biashara na hata kitaaluma.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Urassa uliokuwa ndio ukoo unaotawala katika himaya ndogo ya umangi Keni ya Mkulya, Rombo. Kama jinsi historia inavyotueleza katika ukanda wa Rombo kuna himaya mbili tofauti za umangi zilizokuwa na jina Keni. Kuna Keni ya Shoma iliyopo katika eneo la Shoma ambayo iko katikati ya himaya ya Mengwe na himaya ya Shimbi, halafu kuna hii Keni ya Mkulya ambayo iko katika eneo la Mkulya katikati ya himaya ya Kirua Rombo na himaya ya Mrere. Hii himaya ya umangi Keni ya Mkulya baadaye mwaka 1923 ilikuja kuunganishwa na himaya ya umangi Mrere na kuwa himaya moja iliyoitwa Keni Mrere.

– Hivyo himaya hii ya umangi ya Keni ya Mkulya, Rombo ndio iliyokuwa inatawaliwa na ukoo wa Urassa mpaka mwaka 1923 ilivyounganishwa na himaya ya umangi Mrere ikawa chini ya utawala wa Mangi wa Mrere, Rombo. Mtawala wa mwanzoni zaidi wa himaya hii ndogo ya umangi Keni kutokea katika ukoo wa Urassa inasemekana aliitwa Mangesho ambaye alitawala eneo hili kuanzia katikati ya karne ya 19 na kujaliwa kupata watoto wengi sana ambapo vizazi vyake ndivyo vilivyoendelea kutawala eneo hili mpaka mwaka 1923.

– Mtawala mwingine imara zaidi kutoka kwenye kizazi cha Mangesho wa ukoo wa Urassa aliitwa Towo aliyetawala himaya ya Keni mpaka mwaka 1901 utawala ulipochukuliwa na mtoto wake wa pili wa kiume aliyeitwa Kahumba. Mangi Kahumba wa Keni Mkulya alikuwa mtawala mashuhuri, imara na mwenye msimamo sana na alipata umaarufu mkubwa katika utawala wake kutokana na umahiri wake. Hata hivyo mwaka 1917 Mangi Kahumba wa Keni Mkulya, Rombo alijikuta kwenye tuhuma za uhaini akishirikiana na wamangi wengine wa kichagga kupanga njama za kutaka kuipundua serikali ya waingereza na hivyo kupelekwa kifungoni uhamishoni huko Kismayu, Somalia sambamba na wamangi wengine wote wa kichagga waliokuwa wanahishwa na tuhuma hizo.

– Baada ya Mangi Kahumba kuondolewa madarakani na kupelekwa kifungoni kiti cha umangi wa himaya ndogo ya Keni Mkulya kilikaliwa na mtoto wa kaka yake aliyeitwa Merinyo kutoka kwenye ukoo huo huo wa Urassa. Mangi Merinyo ambaye ni mtoto wa kaka yake mkubwa Mangi Kahumba aliyeitwa Mang’aro aliitawala himaya ndogo ya umangi Keni Mkulya tangu mwaka 1917 mpaka mwaka 1923. Mwaka 1923 utawala wa ukoo wa Urassa kwenye himaya hii ulifikia mwisho pale ambapo himaya hii ya Keni iliunganishwa na Mrere na kuitwa Keni Mrere na kutawaliwa moja kwa moja na Mangi Mrere wakati huo akiwa ni Mangi Pauli Kalula.

– Inasemekana kwamba himaya hii ndogo ya umangi Keni walitakiwa kuunganishwa na himaya ya Kirua Rombo na kutawaliwa kutokea Kirua Rombo lakini walikataa na kuchagua kuunganishwa na himaya ya Mrere ambapo waliweza kuiongezea nguvu zaidi himaya ya Mrere. Himaya hii ya Keni Mkulya, Rombo iliyokuwa inatawaliwa na ukoo wa Urassa inapatikana kwenye eneo ambalo leo hii ni tarafa ya Mashati karibu na eneo maarufu la Mrere, Mashati, Rombo. Baada ya hapo ukoo wa Urassa haujawahi kuusishwa tena na umaarufu mwingine wa kiutawala au kisiasa.

– Hata hivyo ukoo wa Urassa ni ukoo mkubwa uliosambaa na unapatikana kwa wingi sana pia upande wa magharibi wa Uchagga katika himaya ya umangi Machame na Masama na hata maeneo ya katikati ya Uchagga. Ukoo wa Urassa umeendelea kusambaa zaidi na zaidi na unapatikana maeneo ya vijiji vingi vya Uchagga, Kilimanjaro.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kware, Masama.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mungushi, Masama.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mroma Masama.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lemira, Masama.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ng’uni, Masama.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mbweera, Masama.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mboreny, Masama.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sonu, Masama.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Saawe, Massawe.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Roo. Masama.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Uswaa, Machame.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Shari/Uraa, Machame.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nkuu ndoo, Machame.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa kiasi katika kitongoji cha Kimbushi, Nkuu, Machame.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kilanya, Kata ya Lyamungo, Machame.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Lyamungo Kati, Machame.

– Ukoo wa Urassa unapatikana katika kijiji cha Lyamungo Sinde, Machame.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Umbwe, Kibosho.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa uchache sana maeneo ya Mawella, Uru.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kerio, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirua-Rombo, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Keni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kiraeni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Msaranga, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Urassa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kooti, Olele, Rombo.

Ukoo wa Urassa unaonekana kuwa umesambaa sana magharibi na mashariki na hata kwa kiasi maeneo ya katikati lakini taarifa zake na namna ulivyosambaa hazina usahihi. Hivyo tunahitaji mchango zaidi wa mawazo juu ya namna ukoo huu mkubwa na mashuhuri wa wachagga ulivyoweza kupiga hatua mpaka kufikia ulipo sasa. Taarifa hizi zinasaidia kuongeza sana katika maudhui ya koo za kichagga na maudhui ya wachagga kwa ujumla na hivyo kujenga hamasa zaidi, ari na mshikamano kuelekea kufanya makubwa katika maisha.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Urassa.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Urassa?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Urassa?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Urassa?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Urassa una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Urassa wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Urassa kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Urassa?

9. Wanawake wa ukoo wa Urassa huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Urassa?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Urassa?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Urassa?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Urassa kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *