UKOO WA MARO.

– Maro ni ukoo mkongwe sana wa wachagga uliotoa watu mashuhuri sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Ukoo wa Maro wa miaka ya zamani ulitoa wanajeshi hodari sana akiwemo mkuu bora kabisa wa majeshi katika historia ya wachagga Kilimanjaro Mzee Merinyo Maro. Hata miaka ya baadaye ukoo wa Maro ambao umeendelea kusambaa zaidi katika vijiji mbalimbali vya Uchagga katika eneo la katikati ya Uchagga kuelekea mashariki umeendelea kutoa watu mashuhuri ambapo mmoja kati ya watu maarufu sana kutoka kwenye ukoo huu ni Mama Anna Mkapa anayetokea katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi ambaye ni mjukuuu wa mwanaharakati na mbeba maono wa taifa la wachagga Kilimanjaro Mzee Joseph Merinyo Maro.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Maro unaonekana kwamba ulikuwa ni ukoo ambao ulikuwa na jukumu la kutoa ulinzi kwa utawala wa Mangi na kushika nyadhifa za juu zaidi katika serikali. Tunafahamu kwamba Jenerali Merinyo Maro akiwa moja kati ya watu mashuhuri sana na waliowahi kuheshimika sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro ni moja kati ya majenerali waliowahi kuwa na mafanikio makubwa sana. Jenerali Merinyo Maro alikuwa ni sehemu muhimu sana ya mafanikio makubwa kisiasa ya Mangi Rindi Mandara ambaye aliwahi kuwa nguvu kubwa zaidi kisiasa katika historia ya wachagga Kilimanjaro.

– Jenerali Merinyo Maro akiongoza majeshi ya karibu Kilimanjaro yote alikuwa nyuma ya ushindi wa vita nyingi sana za wachagga ndani na nje ya Kilimanjaro vilivyoweza kuja na mafanikio makubwa. Mtoto wake Joseph Merinyo Maro alikuja tena kuwa mwanaharakati mkubwa sana ambaye ndiye mwanzilishi wa chama cha wakulima wazawa cha Kilimanjaro Native Planters Association(KNPA) ambacho ndicho kilichozaa chama cha ushirika cha Kilimanjaro Native Cooperation Union (KNCU) kikiwa ni chama cha kwanza cha ushirika Africa kilicholeta mapinduzi makubwa ya ushirika ndani ya Tanganyika na Afrika mashariki.

– Joseph Merinyo Maro mwenyewe ambaye alikuwa na akili sana na mwenye maono makubwa sana aliwahi kuwa mwenye nguvu kubwa zaidi ya ushawishi Kilimanjaro kuliko hata mtawala yeyote wakati wa utawala wa waingereza. Aliweza kushawishi mabadiliko mengi ya kisiasa Kilimanjaro na hata kubadili watawala kwa namna alivyotaka yeye katika himaya za Machame, Kibosho na Old Moshi na bado akiwa na nguvu kubwa ya ushawishi katika himaya nyingine zote.

– Kwa Uchaggani, Kilimanjaro ukoo wa asili na ngome ya ukoo wa Maro huenda ni katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi au Kidia, Old Moshi ambapo kwa takwimu za kihistoria vizazi vyao vinakwenda mpaka miaka 400 iliyopita wakiwa na jukumu hilo hilo la kuimarisha ulinzi kwa utawala. Hata hivyo ukoo wa Maro umejiimarisha sana pia katika maeneo mengine ya vijiji vya Uru upande wa magharibi na mashariki. Huu ni ukoo wa watu wapambanaji na wenye watu wanaofanya vizuri sana katika biashara na ujasiriamali.

– Ukoo wa Maro uliendelea kusambaa zaidi na unapatikana katika vjiji mbalimbali vya Uchagga Kilimanjaro kuanzia maeneo ya Uru magharibi.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Okaseni, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ongoma, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Msuni, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi sana Mawella Kimanganuni, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana katika kijiji cha Mrawi, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana katika kijiji cha Njari, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shimbwe, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mnini, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kishumundu, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Materuni, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mwasi Kusini, Uru.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa uchache sana maeneo ya vijiji vya Mbokomu.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Maro unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Rauya, Marangu.

Bado tunahitaji taarifa zaidi juu ya ukoo mkongwe sana wa Maro ili kuongeza sana katika maudhui ya ukoo husika na koo za wachagga kwa ujumla. Hivyo tunaomba mchango wa mawazo kwa taarifa zaidi juu ya ukoo huu zitakazosaidia kuongeza hamasa na ari ya kufanya mambo makubwa zaidi kwa ngazi ya ukoo na taifa zima la wachagga kwa ujumla kwa manufaa ya sasa na uzao wa baadaye.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Maro.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Maro?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Maro?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Maro?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mongi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Maro wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Maro kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Maro?

9. Wanawake wa ukoo wa Maro huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Maro?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Maro?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Maro?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Maro kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *