UKOO WA TESHA.

– Tesha ni ukoo mkubwa na maarufu sana wa wachagga waliosambaa maeneo mengi ya Uchaggani, Kilimanjaro kuanzia magharibi kati mpaka mashariki kabisa ya Uchaggani, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye idadi kubwa ya watu wanaopatikana maeneo mengi na wanaofanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali hususan ujasiriamali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Kutoka kwenye historia katika himaya ya umangi Kirua Vunjo wakati wa utawala wa Mangi Pakula mwishoni mwa miaka ya 1600’s kijiji cha Legho kilichopo upande wa mashariki wa Kirua Vunjo kilikuwa kinatawaliwa na ukoo wa Tesha. Mtawala wa eneo hili la mashariki ya Kirua Vunjo ambalo nalo lilikuwa ni himaya ndogo ya Legho katika kipindi cha utawala wa Mangi Pakula lilikuwa linatawaliwa na mtawala aliyeitwa Mangi Ndafu kutoka kwenye ukoo huu wa Tesha.

– Hata hivyo baadaye mwanzoni mwa miaka ya 1700’s wakati wa utawala wa Mangi Singila, Kirua Vunjo mtoto wa Mangi Pakula eneo la Legho lilivamiwa na kujumuishwa ndani ya himaya ya Kirua Vunjo. Mangi Singila alikuwa ameoa dada wa Mangi wa Legho na hivyo kwa msaada wa mke wake huyo Legho iliyokuwa chini ya ukoo wa Tesha ilivamiwa na ukoo wa Tesha ukaangushwa na majeshi ya Mangi Singila wa Kirua Vunjo na hata Mangi wao kuuawa. Huo ndio ukawa mwisho wa utawala wa ukoo wa Tesha katika himaya ya Legho ambayo ilifanywa rasmi kuwa sehemu ya himaya ya umangi Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Tesha umesambaa sana na hivyo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mrawi, Uru.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Njari, Uru.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Shimbwe chini, Uru.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Shimbwe Juu, Uru. Karibu nusu ya kijiji cha Shimbwe Juu ni ukoo wa Tesha.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana katika kitongoji cha Shimbwe Kati, Uru.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kimanganuni, Uru.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kyaseni, Uru.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Maruwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Legho, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mmbahe, Marangu.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mengeni chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Aleni Chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Shimbi Mashariki, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ubaa, Ushiri, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ikuini, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mmomwe, MraoKeryo, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kerio, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kirua-Rombo, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Keni-Mrere, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mrere, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kisale, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Msaranga, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kooti, Olele, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kitowo, Olele, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kingachi, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Leto, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ngaseni, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ubetu, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ture, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Msangai, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Nayeme, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Reha, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nanjara, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kibaoni, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mbomai, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Nesae, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Tesha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kikelelwa, Tarakea, Rombo.

Tunahitaji taarifa zaidi juu ya ukoo wa Tesha ambao unaonekana kuna historia kubwa iliyojificha nyuma yake. Taarifa ambazo zitaongezea kwenye utafiti unaoendelea na kuchangia kujenga hamasa na mshikamano wa wachagga wa ukoo wa Tesha na wachagga kwa ujumla katika kuelekea kufanikisha mambo makubwa katika maisha yao kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja, ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Tesha.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Tesha?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Tesha?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Tesha?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Tesha una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Tesha wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Tesha kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Tesha?

9. Wanawake wa ukoo wa Tesha huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Tesha?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Tesha?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Tesha?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Tesha kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *