UKOO WA KISAKA.

– Kisaka ni ukoo wa wachagga wanaopatikana katika baadhi ya vijiji vya maeneo ya katikati ya Uchaggani, Kilimanjaro. Huu ni ukoo uliosambaa katika vijiji vingi kidogo vya Uchagga unaopatikana katika himaya kadhaa za katikati kuelekea mashariki ya Kilimanjaro.

– Ukoo wa Kisaka ni ukoo wenye watu waliosambaa ndani na nje ya Tanzania wakiwa wanafanya vizuri katika nyanja mbalimbali hususan kitaaluma na hata kwenye utumishi wa umma. Japo sio ukoo mkubwa sana lakini ni ukoo uliojitofatisha na wenye mshikamano mkubwa baina ya wanaukoo ukiwa ni ukoo wa watu makini na wenye msimamo mkali.

– Wachagga wa ukoo wa Kisaka wameendelea kuongeza idadi katika maeneo ya vijiji wanakopatikana lakini huenda chimbuko au asili yake ikawa ni Kirua Vunjo kwani ndiko wanakopatikana kwa wingi zaidi. Hata hivyo hata maeneo ya vijiji vya Old Moshi wanapatikana kwa wingi kiasi pia.

– Hivyo ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Leghomulo, Kilema.

– Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu.

Historia na taarifa kuhusu ukoo wa Kisaka bado ni chache sana japo ni ukoo uliosambaa maeneo mengi, hivyo tunahitaji taarifa zaidi za kuhusiana na ukoo wa Kisaka ili kuongezea katika maudhui ya ukoo huu na koo za wachagga kwa ujumla. Hii itasaidia kuamsha ari zaidi ya mapambano na mshikamano kuanzia kwenye ngazi ya ukoo na jamii yote ya wachagga kwa ujumla kuelekea kufanya mambo makubwa.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kisaka.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kisaka?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kisaka?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kisaka?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kisaka una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kisaka wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kisaka kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kisaka?

9. Wanawake wa ukoo wa Kisaka huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kisaka?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kisaka?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kisaka?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kisaka kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *