UKOO WA NG’UNDA.

– Ukoo wa Ng’unda ni ukoo wa wachagga unaopatikana katika vijiji vya Masama Magharibi kama vile Ng’uni. Huu ni ukoo ambao sio mkubwa sana lakini una watu wengi makini unaoweza kukutana nao katika maeneo mbalimbali.

– Hakuna taarifa za kutosha sana kujua chanzo chake halisi au kama huenda ni tawi la ukoo mwingine mkubwa zaidi unaopatikana katika eneo lolote la Kilimanjaro. Kuna maeneo ya Ng’uni kama vile mtaa wa Nrwashofu na maeneo ya vijiji vya karibu ambapo unaweza kukutana na wachagga wa ukoo huu. Kuna uhitaji mkubwa wa taarifa zaidi kuhusu upana na wa ukoo huu wa Ng’unda.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Ng’unda?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Ng’unda?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Ng’unda?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Ng’unda una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Ng’unda wa kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Ng’unda kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Ng’unda?

7. Wanawake wa ukoo wa Ng’unda huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa ukoo wa Ng’unda?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Ng’unda?

Karibu kwa Maoni na Maswali.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *