*KITABU CHA “MIAKA 700 YA WACHAGGA” – MOSHI.*

– Hiki ndio kipindi katika mwaka ambacho wachagga wanapatikana kwa wingi zaidi Moshi kuliko wakati mwingine wowote. Kwa kutambua hilo tumejitahidi kuhakikisha kwamba nakala kadhaa zinapatikana Moshi japo sio kwa wingi sana kutokana na stock hii ya awamu ya tatu kuelekea kumalizika.

– Hivyo kwa wale wenye kutokea mbali na wale wenye kutaka kununua moja kwa moja, kipindi hiki ikiwa wako Moshi ndio fursa ya kipekee kupata kitabu chetu kinachopatikana Uhuru hotel and Conference Centre, Shanty Town – Moshi.

– Kitabu cha “Miaka 700 ya Wachagga” ni muhimu zaidi kwa wazazi wanaotaka kuwakuza watoto wao katika mitazamo sahihi juu ya historia yao inayoenda kuwaongezea kujiamini kuelekea kufanya mambo makubwa katika maisha.

– Kwa waliosoma kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” wakiwa na mashaka kama kweli kitabu hicho kina uzito huo unaojitambulisha nacho wamekiri kwamba kitabu kimevuka mategemeo yao, kwani wamekutana na mengi ambayo hawajawahi kuyasikia lakini yenye kuvutia, kuelimisha na kubadili mtazamo hususan kutoka mitazamo potofu kwenda mitazamo sahihi.

– Kwa wale ambao hawana kasi katika usomaji au wanahisi wana muda mchache sana lakini wanavutiwa na kitabu, bado wana mengi ya kujifunza kupitia picha za watawala wa tangu karne ya 19 zitakazojenga mtazamo sahihi tofauti na ule potofu wa mwanzoni. Wachina wana msemo wao, “picha moja ni sawa na maneno 1,000.”

– Kununua kitabu hiki pia ndio njia sahihi zaidi ya kuunga mkono kazi hii ya utafiti na uandishi wa mambo ya Wachagga sambamba na tovuti inayohifadhi maudhui haya ya www.wachagga.com ikiwa unavutiwa na makala zinazoandikwa hapa kila siku na ungependa kuona injili hii ikisambaa zaidi na kuleta mabadiliko makubwa hususan ya kimtazamo na baadaye ya kimaisha katika jamii yetu. Hata hivyo utaweza kuelewa mambo mengi zaidi na kwa kina zaidi kupitia kitabu.

– Kwa kununua kitabu hiki pia utahamasisha na wengine wanakiona kwako wanunue na kujifunza na hivyo kupelekea mijadala zaidi yenye tija juu ya mwenendo na hatma ya jamii yetu.

– Kwa wale waliosikiliza mahojiano tuliyofanya pale Moshi fm lakini hawajui wanapata wapi kitabu, kitabu kinapatikana Uhuru hotel(uhuru hostel) Shanty Town, Moshi. Kwa walioko Moshi mjini tunaweza kuwasiliana pia.

Karibuni sana kwa kitabu.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *