UKOO WA MSELE.

– Ukoo ni ukoo mkubwa na maarufu sana Kibosho na unasemekana kuwa ndio ukoo mkongwe zaidi Kibosho kwa kupitia kuhesabu vizazi. Inasemekana kwamba mwanzoni ukoo wa Msele walikuwa wanaishi katika ukanda wa juu wa kijiji cha Uri, Kibosho ambapo kwa sasa ni eneo la msitu wa mlima Kilimanjaro kabla ya kushuka na kuweka makazi ya kudumu katika kijiji cha Uri.

– Kutoka kwenye historia inafahamika kwamba Mzee wa mwanzoni zaidi wa ukoo wa Msele alitwa Ngiai na mzee aliyefuata aliitwa Kiwoso ambaye ndiye jina Kibosho lilitokea kwake. Mzee Kiwoso kutoka kwenye ukoo wa Msele alipata umaarufu sana kiasi kwamba kwa miaka hiyo ya zamani watu walilitaja eneo la Kibosho kwa jina la Kiwoso mwenyewe, wa ukoo wa Msele.

– Ukoo wa Msele umetoa watu mbalimbali waliopata umashuru katika historia. Mojawapo ya watu mashuhuri katika historia ya wachagga Kilimanjaro kutoka kwenye ukoo wa Msele ni mke wa Mangi Lokila wa Kibosho aliyeitwa Manka ambaye ndiye alikuwa mtawala wa Kibosho baada ya mume wake Mangi Lokila kufariki na alisimana imara sana katika kiti cha utawala. Manka alikuwa ni kati ya wanawake wachache sana kuwahi kukalia kiti cha umangi katika historia ya wachagga Kilimanjaro.

– Wachagga wa ukoo wa Msele waliendelea kuongezeka idadi na kutokea kijiji cha Uri, Kibosho walisambaa kwenye vijiji vingine.

– Hivyo ukoo wa Msele wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Uri, Kibosho.

– Ukoo wa Msele wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uchau, Kibosho.

– Ukoo wa Msele wanapatikana katika kijiji cha Maua, Kibosho.

– Ukoo wa Msele wanapatikana katika kijiji cha Otaruni, Kibosho.

– Ukoo wa Msele wanapatikana katika kijiji cha Omarini, Kibosho

– Ukoo wa Msele wanapatikana katika kijiji cha Dakau, Kibosho.

– Ukoo wa Msele wanapatikana katika vijiji vya kata ya Kindi, Kibosho.

– Ukoo wa Msele wanapatikana katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Msele wanapatikana katika kijiji cha Manushi, Kibosho.

– Ukoo wa Msele wanapatikana katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.

– Ukoo wa Msele wanapatikana katika kijiji cha Kirima Kati, Kibosho.

Ukoo Msele pamoja na kwamba ni ukoo wenye historia kubwa lakini bado kuna uhaba mkubwa wa taarifa za kuhusu ukoo huu. Tunahitaji mchango zaidi wa mawazo kupata taarifa nyingi kwa ajili ya utafiti na ili kuongeza maudhui zaidi ya kuhusu ukoo husika.

Karibu kwa mchango zaidi wa mawazo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Msele?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Msele?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Msele?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Msele una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Msele wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Msele kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Msele?

9. Wanawake wa ukoo wa Msele huitwaje?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Msele?

11. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Msele?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na ukoo wa Msele?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Msele kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *