UKOO WA KIRUNDWA.

– Ukoo wa Kirundwa au wakati mwingine huitwa Kihundwa ni ukoo mdogo unaopatikana kwa wingi zaidi katika kijiji cha Mese, Siha/Sanya Juu. Ukoo wa Kirundwa unapatikana pia kwa uchache katika vijiji vingine vya Siha/Sanya Juu.

– Kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi inasemekana kwamba ukoo wa Kirundwa huenda ni tawi la ukoo wa Munuo wenye asili yake katika kijiji cha Kyuu, Masama kutokana na kwamba moja katika ya matawi ya ukoo wa Munuo huitwa Munuo-Kirundwa. Hata hivyo hili halina ushahidi wa moja kwa moja.

– Tunahitaji mchango wa mawazo zaidi kufahamu undani wa ukoo huu wa Kirundwa ambao sio maarufu sana na watu wengi hawajui na wengine hawaamini kwamba ni moja ya koo za kichagga.

Tunahitaji mchango wa mawazo zaidi juu ya ukoo huu Kirundwa ambao ni mkongwe sana magharibi ya Kilimanjaro.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kirundwa?

2. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kirundwa?

3. Kama wewe ni wa ukoo wa Kirundwa una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

4. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo huo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

5. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kirundwa?

6. Wanawake wa ukoo wa Kirundwa huitwaje?

7. Una rafiki yako yeyote wa ukoo wa Kirundwa?

8. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kirundwa?

Karibu kwa Maoni na Maswali.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *