UKOO WA MSAKI.

– Msaki ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi katika eneo la katikati ya kuelekea mashariki ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Msaki ni ukoo mkubwa uliosambaa katika vijiji vingi vya Uchagga, Kilimanjaro katika maeneo ya katikati kuelekea mashariki.

– Ukoo wa Msaki ni ukoo wenye vipaji mbalimbali hivyo una watu wengi wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali kama vile ujasiriamali na taaluma mbalimbali. Hivyo Msaki ni ukoo uliotoa madaktari maarufu na wajasiriamali na wafanyabiashara maarufu. Ukoo huu una watu mashuhuri wanaofanya vizuri ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Japo bado hatujaweza kupata uhakika haswa wa chimbuko halisi la ukoo wa Msaki lakini ukoo huu uliendelea kusambaa na unapatikana maeneo ya vijiji vingi vya Kilimanjaro kuanzia katikati kuelekea katikati mashariki.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kimanganuni, Uru.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Okaseni, Uru.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Njari, Uru.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mnini, Uru.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mwasi-Kusini, Uru.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Korini Kusini, Mbokomu.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Manu, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Yamu, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Msaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu.

Ukoo wa Msaki ni ukoo wenye watu wengi mashuhuri lakini bado kuna mengi sana yaliyojificha kutoka kwenye ukoo huu. Tunahitaji mchango mkubwa wa mawazo kutoka kwako kuhusiana na ukoo huu maarufu wa Msaki. Taarifa hizi zitachangia sana kuongeza maudhui ya koo za wachagga na maudhui ya wachagga kwa ujumla sambamba na kujenga hamasa na mshikamano katika jamii ya wachagga kuelekea kufanya mambo makubwa kwenye maisha.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Msaki.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Msaki?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Msaki?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Msaki?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Msaki una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Msaki wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Msaki kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Msaki?

9. Wanawake wa ukoo wa Msaki huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Msaki?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Msaki?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Msaki?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Msaki kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. NAPENDA KUJUA KUHUSU UKOO WA MSOKA UNAOPATIKANA MAENEO YA URU NA KCMC NA MAENEO MACHACHE YA PASUA AU SHABAHA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *