UCHAWI KWA WACHAGGA/(USAWI)

Je, Wachagga wa Leo Tuko Katika Nafasi Gani Tunapozungumzia Suala Zima La Uchawi? Katika Kitabu Cha Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani na Ahera, Tulichoandikiwa Wachagga na Mangi Petro Itosi Marealle Miaka Ya 1940s, Ambacho Amejaribu Kuzungumza Kwa Mapana Kuhusu Mambo Mengi Yanayotuhusu Wachagga Amezungumzia Pia Suala Zima La Uchawi kwa Wachagga. Mangi Petro Itosi Marealle, Mtoto wa Mangi Ndegoruo Marealle Alikuwa ni Mchagga Msomi na Aliyekuwa na Maono Makubwa, Hivyo Aliweza Kuandika Baadhi Ya Mambo Ambayo ni Msaada Mkubwa Kwetu Wachagga wa Vizazi Vya Mbele Tunapokabiliana na Changamoto Mbalimbali za Hii Dunia.

Wachagga ni Watu Ambao Walikuwa Wanaogopa Sana Uchawi Miaka Ya Zamani Sana Huko Karne Ya 19 Lakini Walikuwa Na Bidii Ya Kutafuta Utatuzi wa Matatizo Yao Mbalimbali, Hivyo Walijitahidi Kujiuliza Asili Ya Uchawi na Namna Wataweza Kuiondoa Hatari Hiyo Kwenye Maisha Yao. Mangi Petro Itosi Marealle Anatuambia Mpaka Kufikia Mwanzoni mwa Karne Ya 20 Hofu za Kuogopa Uchawi na Wachawi Kwa Wachagga Zilikuwa Zimepungua Sana na Zinaelekea Kutoweka kwa Sababu Wachagga Wengi Walifika Mahali na Kujua Kwamba Habari za Uchawi Sio Halisia na Waganga ni Watu Waongo.

Ni Miaka Ya 1930s Ambapo Mangi Petro Itosi Marealle Anaandika Kwamba Habari za Uchawi kwa Wachagga Zinatoweka na Zitakwisha Kabisa. Ukweli ni Kwamba Uchawi Sio Kweli ni Habari za Kujaza Hofu Watu Kwa Maslahi Ya Waganga na Watu Wengine Wanaonufaika na Hofu Hizo. Mangi Petro Itosi Marealle Anaandika Jinsi Waganga Wanatumia Mbinu za Uongo Kuaminisha Watu Kwamba Wanawatibu na Kuwaepusha na Uchawi na Watu Kuamini Na Kugeuka Watumwa Wao. Hivyo Wachagga Kama Jamii Tulishafikia Hatua Kwamba Uchawi Tulikuwa Tumeondoa na Tulikuwa Tunaelekea Kuufuta Kabisa Kilimanjaro, Lakini ni Bahati Mbaya Kwamba Baada Ya Kujiunga na Nchi Ya Tanzania na Kukutana na Jamii Nyingine Zinazoamini Sana Uchawi na Uganga Wengi Tumerudi Tena Nyuma Kufanana na Babu Zetu wa Karne Ya 19.

Kiuhalisia ni Kwamba Jamii Zinazoamini Uchawi ni Jamii Zenye Fikra Duni Sana na Maendeleo Yao Huwa Duni Sana Siku Zote. Ni Bahati Mbaya Zaidi Kwamba Wapo Watu Wanaonufaika na Hofu Hizi za Uchawi Kama Waganga wa Kienyeji na Manabii wa Uongo Hivyo Imekuwa Rahisi Kututumbukiza Tena Wachagga Katika Imani za Kichawi Kwa Sababu Tumechagua Kuwaamini Watu Wao. Mangi Petro Itosi Marealle Anasisitiza Kwamba Imani Hizi za Kichawi Zinaturudisha Nyuma Kimaendeleo na Tunatakiwa Kuziepuka Kwa Gharama Yoyote Kwani Hazitusaidii na Hazina Uhalisia Pia. Ukweli ni Kwamba Hakuna Mtu Anayeweza Kukuloga Zaidi Ya Hofu Zako Mwenyewe, Hakuna Mtu Anaweza Kukudhuru Kichawi Kama Unavyodhani Na Kitendo Cha Kuwaza Hivyo ni Dalili za Wewe Kuwa Duni Kifikra. Jamii Zilizostaarabika na Kuendelea Hofu za Uchawi Huondoka Kwa Sababu Hofu Hizo Sio Halisi.

Ni Nadra Sana Kumkuta Mzungu Anaogopa Uchawi, Lakini Karibu Kila Mmakonde Utakuta Anaamini Uchawi, Umewahi Kujiuza Kwa Nini?, Jibu ni Uduni wa Fikra. Mtu Yeyote Yule Hata Kama ni Kiongozi Wako wa Dini Anayekujaza Hofu Zozote za Uchawi Huyo ni Mtu Anayetaka Kuendelea Kukutumikisha na Kwa Vyovyote Vile Kuna Namna Unamfaidisha, Jitahidi Umuepuke. Mangi Petro Itosi Marealle Ameweza Kutuambia Jinsi Waganga Walivyokuwa Wanatumikisha Watu Kwa Hila. Wachagga Tulishaachana na Habari Za Uchawi Zaidi Ya Miaka 100 Iliyopita, Kabla Hatujarudi Nyuma Kwa Kuungana na Jamii Ambazo Bado Utapeli wa Mambo Ya Kishirikina Uko Juu na Ndio Maana Utakuta Hakuna Waganga Wa Kienyeji Wachagga Ni Kwa Sababu Hawakuhitajika Tena.

Toka Zamani Tumekuwa Tukisikia Mganga Anatoka Tanga au Anatoka Mombasa Lakini Sio Mchagga. Hata Hivyo Wachagga Waliwapuuza Sana Watu Hawa Miaka Ya Zamani Kwa Kuwa Walijua Ni Watu Matapeli. Bibi Yangu Alikuwa Akiniambia (Wahanga Walembi), Akimaanisha Waganga ni Watu Wadanganyifu na Waongo. Ndio Maana Utakuta Jamii Ambazo Imani za Kishirikina Ziko Juu na Waganga Wengi Wanatoka Huko Ziko Duni Sana Kimaisha. Hata Huko Sumbawanga Kunakosifika Kwa Uchawi Ni Moja Kati Ya Sehemu Maskini Kabisa Tanzania, Hii Ni Kwa Sababu Imani Hizi Zinatia Watu Hofu Wanakuwa Hawafanyi Maendeleo.

Ni Habari za Kusikitisha Kwamba Baadhi Ya Wachagga wa Leo Wamerudi Huko Tena. Japo Hatuwezi Kuwalaumu Moja kwa Moja Kwa Sababu Jamii Ambazo Tumekuja Kuishi Nazo Hazijawahi Kuondoka Kwenye Mambo Hayo Ya Ushirikina na Mbaya Zaidi Wameibuka Wajanja wa Kunufaika na Fursa za Hofu za Watu Kwa Kuwaaminisha Kwamba Hawako Salama Dhidi Ya Wachawi.

USHIRIKINA UPO

Kinachofanya Hofu za Uchawi Kuaminika Kwamba ni Kitu Cha Kweli ni Kama Anavyotueleza Mangi Petro Itosi Marealle Kwamba Ni Hila Za Waganga, Wanaohalalishwa na Manabii wa Uongo. Kuna Watu Wanaenda kwa Waganga na Kupewa Huo Unaoitwa ni Uchawi na Masharti Ya Namna Ya Kuutumia. Watu Hawa Wanaamua Kufanya Hivi Kwa Sababu Ya Wivu, Chuki, Roho Mbaya Au Visasi Dhidi Ya Maadui Zao, Ambao Ni Udhaifu Tulionao Binadamu Wengi. Sasa Watu Hawa Wanapofumaniwa Wakitekeleza Maagizo Ya Waganga Ndio Huonekana Kama ni Wachawi Lakini Hata Wao Wanakuwa Wamedanganywa Tu na Waganga Lakini Kiuhalisia Wanachofanya Hakina Madhara Yoyote Kwa Mtu Yeyote.

Najua Kwamba Hapo Kijijini Kwenu Kuna Mbibi au Mmama Fulani Labda Bibi Mashirima, Ambaye Unaamini Ni Mchawi na Analoga. Ukweli ni Kwamba Huyo Mtu Hana Uwezo wa Kufanya Hayo Unayofikiri Japo Kweli Amewahi Kuonekana Akifanya Mambo Yasiyoeleweka, Ila Huo ni Ushirikina Tu Aliodanganywa na Mganga Kwamba Utaleta Matokeo Fulani Lakini Ni Uongo Mtupu Japo Jambo Hilo Litapelekea Yeye Kunyanyapaliwa Sana na Watu Kwa Kutuhumiwa ni Mchawi.

TUSIWAOGOPE WACHAWI BALI TUWAPUUZE.

Kiuhalisia Wachawi ni Watu Ambao Wanaweza Kuwa Hawapendi Maendeleo Yako Lakini Hawawezi Kufanya Chochote Kukuzuia, Hata Kama Kweli Wamepewa Maelekezo Ya Kupiga Ramli na Mganga Ni Kazi Bure Tu. Wala Huhitaji Kuombewa na Nabii Ili Usilogeke, Unapaswa Tu Kuachana na Hofu za Kulogwa au Kudhurika Kichawi na Unakuwa Upo Salama.

Najua Hili Sio Jambo Rahisi Hasa Kwa Watu Ambao Wameishi Miaka Yao Yote Kwa Hofu za Wachawi, Najua Hili Sio Jambo Rahisi Kama Kila Siku Unamsikiliza Mchungajji Wako Anayekwambia Ni Jinsi Gani Wachawi Wanakuwinda Kila Siku au Freemason Wamechukua Nyota Yako, Najua Hili Ni Gumu Zaidi Kwa Wanawake Ambao Kisaikolojia Hisia Zao Huwa Ziko Juu Zaidi Ukilinganisha na Wanaume na Najua Hili Sio Rahisi Kwako Kijana Ambaye Tangu Umezaliwa Umekuwa Ukiaminishwa Kwamba Mashirima ni Mchawi na Ulishapewa Ushahidi Wote Uliouamini.

Lakini Leo Nakwambia Mangi Petro Itosi Marealle Yuko Sahihi Kabisa na Ameweza Kutusaidia Sana Kwa Kutuonya Mapema Wachagga Juu Ya Utapeli wa Hii Dunia, Uchawi Sio wa Kweli na Unafanya Kazi Kwa Watu Wenye Fikra Duni Peke Yake, Hao Wanaokutia Hofu za Uchawi Wanalenga Kukuibia.

Wachagga Kama Jamii Nyingine Zilizotangulia Kuwa Makini Duniani Tulishaachana na Habari za Uchawi Lakini Tunarudishiwa Tena Baada Ya Kujichanganya na Jamii Nyingi Duni Kifikra. Ondoa Hofu, Songa Mbele na Maisha Hakuna Cha Kukuzuia.

Tuachane na Hofu za Wachawi Ambazo Hazina Uhalisia Lakini Zinaturudisha Nyuma.

Karibu Kwa Swali, Maoni, Ushauri.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *