FALSAFA YA WACHAGGA(CHAGGA PHILOSOPHY)

Falsafa za Jamii Mbalimbali Duniani Ndizo Huzaa Tamaduni Nyingi za Jamii Husika na Kuamua Hatima Za Kisiasa, Kiuchumi, Kijamii, Kiteknolojia, Kitaaluma na Hata Kiroho. Je, Tunaweza Kuifahamu Falsafa Ya Wachagga au za Wachagga Ambazo Zimeathiri Mwenendo wa Maisha Ya Mchagga?

Je Kuna Wanafalsafa wa Kichagga Wanaofahamika Ambao Walichangia Katika Kutengeneza au Kuboresha Falsafa Hizi?

Tunajua Kwamba Dini zote, Siasa, Taaluma Mbalimbali na Kila Kitu Kinachohusisha Fikra na Mifumo Mbalimbali Duniani ni Mazao Ya Falsafa Mbalimbali za Zamani Zaidi Ambazo Zilibuniwa na Kuendelezwa na Watu wa Jamii Husika. Kwa Mfano Dini Ya Kikristo ni Matokeo Ya Muunganiko wa Falsafa na Historia za Jamii Nyingine za Watu wa Mashariki Ya Kati na Ulaya Ambayo Ilianza Kupata Umaarufu Kwa Kasi Sana Mwanzoni Mwa Milenia Ya Kwanza na Hasa Baada Ya Kufanywa Dini Rasmi Ya Dola Ya Rumi Wakati wa Mtawala Constantine(Emperor Constantine) Mwaka Karne Tatu Baadaye. Tangu Hapo Dini Ya Kikristo Ikaendelea Kuwa na Ushawishi Mkubwa Ulaya na Kuathiri Tamaduni na Maisha Ya Ulaya Kwa Zaidi Ya Miaka 1500 sasa.

Kuna Falsafa Kadhaa Ambazo Zilijumuishwa Kuweza Kupatikana Dini Ya Kikristo Lakini Baada Ya Dini Hii Kufanywa Dini Rasmi na Dola Ya Rumi Falsafa Zaidi Zilizozidi Kuongezwa na Kuboreshwa Zilitengeneza Sura Ya Ukristo wa Kanisa Katoliki, na Baada Ya Harakati Za Waprotestants, Miaka Zaidi Ya 1,000 Baadaye Falsafa Zaidi Ziliongezwa Ambazo Zilileta Picha Ya Ukristo wa Kiprotestant na Hata Kubadili Kwa Kiasi Ukatoliki. Kwanza Historia Takatifu Iliyochukuliwa Ni lle Ya Wayahudi Kwa Sababu Ukristo Ulianza Kama Mabadiliko/Reform Ya Dini Ya Wayahudi, Hivyo Historia Ya Wayahudi Ikawa Ndio Historia Takatifu.

Baadaye Zikaingizwa Falsafa za Wayunani wa Kale/Ancient Greece Philophies Kama Falsafa Ya Ustoa/Stoicism Philosophy, Falsafa ya Usiniko/Cynicism Philosopy, Falsafa Ya Epicurean/Epicureanism Philisophy n.k., Mfano wa Falsafa Ya Ustoa/Stoicism Philosophy Katika Ukristo na Hata Uislamu Ambao Kwa Sehemu Kubwa Ulikopi Kutoka Kwenye Ukrito ni Maombi Ya Kufunga, Hii ni Moja Ya Falsafa za Uvumilivu Ambazo Zilianzishwa na Kutekelezwa Wastoa wa Uyunani Ya Kale, Miaka Zaidi Ya 300 Kabla Ya Ukristo. Au Ile Falsafa Ya Uza Mali Zako Uwape Maskini na Kisha Ukafanye Kazi Takatifu, Hii ni Falsafa ya Cynicism Iliyojumuishwa Kwenye Ukristo. Kwa Sababu Wayunani wa Kale Ndio Walikuwa Wasomi na Wanasayansi Wakubwa Kabla Ya Dola Ya Rumi Kukua Hivyo, Dola Ya Rumi Ilipokuja Kuiangusha Dola Ya Wayunani au Wagiriki wa Kale Bado Walikuwa na Ushawishi Mkubwa Ndani Ya Rumi na Falsafa Zao Ndio Zilitumika Kufanya Mapinduzi Mengi Ya Kitaaluma na Ya Kiroho Ndani Ya Dola Ya Rumi.

Falsafa za Wayunani wa Kale Kama Wakina Pythagorus, Socrates, Plato, Aristotle n.k., Ndizo Zilisaidia Sana Kukuza Dini Ya Kikristo na Hata Taaluma Nyingine Ndani Ya Dola Ya Rumi. Wanafalsafa wa Kanisa Katoliki Kama Mtakatifu Agustino wa Hippo/St. Augustine of Hippo, Mtakatifu Tomasi wa Aquino/St. Thomas Aquinas, Mtakatifu Jerome/St. Jerome, Mtakatifu Ambrose/St. Ambrose, Mtakatifu Benectine n.k., Ambao Walichangia Sana Kuongeza Kwenye Falsafa Ya Kanisa Katoliki Walijifunza Falsafa Hizi Nyingi Kutoka Kwa Wanafalsafa wa Uyunani Ya Kale. Mtakatifu Agustino wa Hippo/St. Augustine of Hippo wa Kanisa Katoliki Ambaye Anaheshimika Sana na Madhehebu Yote Ya Kikristo na Anatambulika Pia na Waprotestant, Amechangia Falsafa za Kanisa Katoliki Kwa Sehemu Kubwa Kuliko Mwanafalsafa Mwingine Yeyote, Falsafa Zake Nyingi Amejifunza Kwa Plato, Mwanafalsafa wa Uyunani Ya Kale, na Falsafa Kama Ya Uzima wa Milele Alijifunza Kwa Mwanafalsafa wa Zamani Zaidi wa Uyunani Ya Kale Ambaye Pia Alikuwa Mwanahisabati Aliyeitwa Pythagorus. Vile vile Mwanafalsafa Mwingine wa Kanisa Katoliki Mtakatifu Tomasi wa Aqino/St. Thomas Aquinus, Falsafa Zake Nyingi Zilizochangia Kubadili Taswira Ya Kanisa Katoliki Alizijifunza Kutoka Kwa Mwanafalsafa Aristotle wa Uyunani Ya Kale. Kuanzia Vita, Sayansi, Dini, Uchumi, Taaluma, Teknolojia, Lugha, Tamaduni, n.k., Zimezalishwa na Falsafa Fulani za Jamii Husika au Hata Kuchanganyika na Jamii Nyingine.

Huko Mashariki Ya Mbali au Asia Nao Wana Vitu Vingi Vilivyotokana na Kuanzishwa na Falsafa Zao na Wanafalsafa Wao Pia Kama Budhism, Confusianism, Hinduism, Taoism, Shintoism na Vitu Vingine Vingi Sana Vilivyochangia Kwenye Tamaduni Zao. Je, Sisi Wachagga Tunaweza Vipi Kufuatilia Falsafa Zetu Ambazo Zimetufikisha Hapa Tulipofika Kama Hao Wenzetu?, Na Je Kuna Vitu Tunaweza Kuandika Kutokea Hapo Kuboresha Zaidi Maeneo Mengine Ambayo Zimetokana na Sisi?, Tukumbuke Falsafa Zinaingia Kwenye Kila Nyanja Ya Maisha.

Kwa Maoni Yangu Nafikiri Tunaweza.

Mwanataaluma na Mmisionari wa Kijerumani Dr. Bruno Guttman Ameweka Kwenye Maandishi Mambo Mengi Sana Kuhusu Wachagga na Kila Kitu Kizuri au Kibaya Kuhusu Sisi. Akishirikiana na Wanataaluma Wengine wa Kichagga wa Zamani Hizo Kama Akina Mlasany Njau na Wengine Wengi Aliowataja Kwenye Maandiko Yake. Pia Kuna Baadhi Ya Mambo Yaliamuliwa na Mangi Yaendelee au Yabadilike, Kwa Mfano Mangi Rindi Mandara Kuna Baadhi Ya Mambo Aliamuru Yasitishwe na Mengine Yaendelea Ambapo Alikuwa Anajaribu Kuboresha, Dr. Bruno Guttman Amejaribu Kuandika Sana Pia Mambo Haya. Dr. Bruno Guttman Aliweza Kuandika Vitu Vingi Sana Ambavyo Tunapaswa Kujifunza na Kuandika Mambo Yetu Mengi Ambayo Tunaweza Kujivunia na Hata Kujivunia Kwa Faida Ya Vizazi Vya Mbele. Dr. Bruno Guttman Amekuwa Kam Mtakatifu Agustino wa Hippo kwa Wakristo kwa Ujumla Kwa Sababu Ametuandikia Zaid Ya Vitabu 400 na Makala Nyingine Nyingi Sana Kuhusu Sisi Wachagga.

Japo Pia Watu Kama Kina Petro Itosi Marealle, Somebody Njau na Wanazuoni Wengine wa Kichagga Walijitahidi Kuandika Kwa Kiasi Falsafa Zetu za Miaka Ya Nyuma.

Kazi Imebaki Kwetu.

Karibu kwa Maswali au Maoni Zaidi.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *