UKOO WA KISANGA.

– Kisanga ni ukoo wa wachagga unaopatikana maeneo ya vijiji kadhaa vya Uchaggani, Kilimanjaro. Ni ukoo uliotoa wachagga wengi mashuhuri na unapatikana katika vijiji vya katikati ya Uchagga kwa wingi na kwa kiasi katika vijiji vichache vya mashariki. Hata hivyo ukoo wa Kisanga unapatikana kwa wingi zaidi katika vijiji vya himaya ya Mbokomu iliyokuja kuwa sehemu ya himaya ya Old Moshi.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Kisanga unaonekana ulikuwa ni ukoo wenye nguvu sana katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi na ulikuwa ukitawala katika kijiji hiki. Mzee wa zamani zaidi anayekumbukwa na historia aliyekuwa mtawala wa kijiji hiki cha Mahoma, Old Moshi kutoka kwenye ukoo wa Kisanga aliitwa Poloso na inakadiriwa kwamba aliishi katika miaka ya mwishoni mwa karne ya 17 yaani miaka ya mwishoni mwa 1600.

– Baadaye ukoo wa Kisanga ambao ulikuwa mashuhuri sana eneo hili uliendelea kutoa wachili wa kijiji hiki na kwingine ulikopatikana kama wasaidizi wa Mangi. Ukoo wa Kisanga umeendelea kutoa watu kadhaa mashuhuri wanaofanya vizuri maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. Ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi kiasi. Moja kati ya watu mashuhuri kutokea kwenye ukoo huu ni aliyewahi kuwa Jaji Mkuu Robert Kisanga kutokea Mbokomu.

– Ukoo wa Kisanga uliendelea kusambaa zaidi na kupatikana maeneo zaidi ya Uchagga kuanzia katika baadhi ya maeneo ya Uru kwa uchache sana.

– Ukoo wa Kisanga unapatikana kwa wingi sana katika Kijiji cha Korini Kusini, Mbokomu hususan maeneo ya Kiwalaa.

– Ukoo wa Kisanga unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Korini Juu, Mbokomu kama maeneo ya Fukeni n.k.,

– Ukoo wa Kisanga unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Korini Kati, Mbokomu.

– Ukoo wa Kisanga unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tema, Mbokomu.

– Ukoo wa Kisanga unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Kisanga unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Kisanga unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Kisanga unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

– Ukoo wa Kisanga unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mawanjeni, Mwika.

Maudhui zaidi kuhusiana na ukoo wa Kisanga yanahitajika ili kuongeza katika maktaba sambamba na maudhui zaidi kuhusiana na koo za wachagga kwa ujumla. Maudhui haya yatasaidia katika tafiti zaidi zinazoendelea sambamba na kuhamasisha mshikamano zaidi baina ya wanaukoo na wachagga kwa ujumla kuelekea kufanikisha mambo makubwa katika ngazi ya mwanaukoo mmoja mmoja, ngazi ya ukoo na wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kisanga.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kisanga?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kisanga?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kisanga?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kisanga una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kisanga wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kisanga kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kisanga?

9. Wanawake wa ukoo wa Kisanga huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kisanga?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kisanga?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kisanga?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kisanga kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *