WACHAGGA NA MTI MTAKATIFU WA ISALE

MCHAGGA HALISI Popote Utakapoweka Makazi Lazima Uoteshe Masale Kuashiria Ni Makazi Ya Mchagga Na Kutujulisha Wachagga Wenzako Kwamba Wewe Ni Mwenzetu.

Jani La Isale Limetufanyia Mengi Sana, Limesaidia Kutatua Migogoro Na Vita Ambazo Kama Zingepiganwa Pengine Babu Yako Ambaye Wewe Umetokea Kwenye Vizazi Vyake Angepoteza Maisha Kwenye Vita Hiyo Na Wewe Usingekuwepo Leo. Hata Uhasama Kati Ya Machame Na Kibosho Isale Lilihusika Katika Kuumaliza.

Tuwe Na Shukrani Kwa Mti Huu Mtakatifu Na Uliotufanyia Mengi Unaoashiria Amani Na Maelewano. Mzee Wangu Mmoja Alimtembelea Rafiki Yake Mchagga Mwenye Makazi Yake Huko Amerika Ya Kati Katika Nchi Ya Costa Rica Na Anasema Alikuta Amepanda Masale Kwake, Na Licha Ya Kuoa Mwanamke Wa Huko Lakini Alikuwa Na Maisha Ya Kichagga Sana Hasa Upande wa Vyakula Na Vinywaji.

Bibi Yangu Alikuwa Akimtembelea Mtoto Wake Yeyote Nje Ya Kilimanjaro Lazima Aende Na Mimea Ya Masale Kwa Ajili Ya Kupanda Katika Makazi Hayo Ya Ugenini, Kuweka Alama Kwamba Ni Makazi Ya Mchagga. Wangapi Tumejumuisha Masale Kwenye Bustani Zetu Katika Makazi Yetu Mapya Katika Miji Mingine?

MASALE YA MPAKANI
MASALE YA SHAMBANI

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *