UKOO WA SHAYO.

– Shayo ni ukoo maarufu sana wa wachagga unaopatikana maeneo mengi sana ya Uchaggani, Kilimanjaro hususan kuanzia katikati mpaka mashariki kabisa. Ukoo wa Shayo ni ukoo wenye idadi kubwa sana ya watu na umeweza kutoa wachagga mbalimbali mashuhuri wanaofanya vizuri sana maeneo tofauti tofuati.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Shayo unazungumziwa kwamba ulikuwa unapatikana Marangu na walikuwa ni wachagga mahodari wa kufua vyuma kama koo nyingi mashuhuri za ufuaji vyuma kama vile Makundi, Malisa, Chuwa n.k., Historia inasema kwamba wamangi wa Kilema na hususan Mangi Rongoma ndio walihamasisha ukoo wa Shayo kuhamia Kilema kwa lengo la kusaidia utengenezaji wa silaha bora na zenye nguvu.

– Ukoo wa Shayo walihamia Kilema kutokea Marangu na kuimarisha kiwanda cha utengenezaji silaha kwa teknolojia ya kufua vyuma na hivyo kuiongezea nguvu Kilema kijeshi iliyoweza kuiangusha na kuitawala Marangu na hata Vunjo yote. Ukoo wa Shayo Kilema waliendelea kupata umaarufu mkubwa na kuheshimika sana kwa ubunifu huo na vipaji hivyo vilivyokuwa muhimu sana Uchaggani kote katika kuimarisha tawala za himaya za wachagga.

– Upande wa mashariki huko Rombo ukoo wa Shayo wanaonekana kuwa na chimbuko zaidi katika kijiji cha Reha, Tarakea, Rombo ambapo zamani ilikuwa ni sehemu ya Usseri. Ukoo huu wa Shayo umeendelea kusambaa zaidi katika vijiji zaidi vya Uchaggani na wanapatikana kwa wingi sana kwa baadhi ya vijiji na kwa uchache katika vijiji vingine. Wachagga wengine wa ukoo wa Shayo pia hujiita ukoo wa Manjira ambao ni ukoo huo huo wa Shayo.

– Hivyo kutokana na kusambaa huko ukoo wa Shayo unapatikana katika kuanzia katika kijiji cha Lukani, Masama.

– Ukoo Shayo unapatikana katika maeneo ya kijiji cha Mawela, Uru.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mrawi, Uru.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Njari, Uru.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa kiasi maeneo ya Mbokomu.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo Shayo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Manu, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana katika kijiji cha Yamu, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Legho, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ngangu, Kilema.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Marawe Kyura, Kilema.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kimaroroni, Kilema.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Rauya, Marangu.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mshiri, Marangu.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kyala, Marangu.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimbogho, Mamba.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi kiasi katika eneo la Mrieny, Mamba.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Shayo unapatikana katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa kiasi katika vijiji vya tarafa ya Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Aleni chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Maharo, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kerio, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mmomwe, Mrao, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirongo Juu, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Samanga, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ubetu, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ngasseni, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Leto, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kingachi, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kahe, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Reha, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Urauri, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msangai, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Nayeme, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Nesae, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mbomai, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Shayo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nanjara, Tarakea, Rombo.

Ukoo wa Shayo ni ukoo maarufu na mashuhuri sana lakini bado kuna uhaba mkubwa wa taarifa kuhusiana na ukoo huu, hivyo tunahitaji kufahamu zaidi juu ya ukoo wa Shayo ili kuongezea katika utafiti unaoendelea. Taarifa hizo zitatusaidia katika kuongezea kwenye maudhui zaidi ya ukoo huu na koo za wachagga kwa ujumla ili kujenga ari, hamasa na mshikamano dhabiti kuelekea kufanikisha makubwa kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja, ngazi ya ukoo na ngazi ya jamii ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Shayo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Shayo?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Shayo?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Shayo?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Shayo una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Shayo wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Shayo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Shayo?

9. Wanawake wa ukoo wa Shayo huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Shayo?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Shayo?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Shayo?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Shayo kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. Benedict Jo hn kombe says:

    Naomba jamani kama kuna mwenye historia ya ukoo WA KOMBE Kuaanzia mamba atuambie mm Niko KOMBE Niko kirua vunjo ila naambiwa chimbuko letu ni mamba

    1. Ndio Kombe wako mpaka Mwika na Kilema pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *