MICHAEL NGALEKU SHIRIMA.

One of the Greatest Sons of Kilimanjaro.

– Wachagga na Sifa Ya Kipekee Sana Kama Jamii Ya Wazawa Ndani Ya Nchi Hii Inayofanya Vizuri Sana Kwenye Sekta Binafsi. Pamoja na Mitazamo Hasi na Chuki za Baadhi Ya Watu Kwa Jamii Hii Bado Kwa Sehemu Kubwa Ndio Viongozi Katika Maeneo Mengi Kwenye Sekta Binafsi Nchini.

Leo Kuna Huyu Mchagga Mzalendo na Mjasiriamali Msomi Aliyeacha Alama Kubwa Sana Katika Sekta Binafsi Tanzania Kwenye Sekta Ya Anga. Inasemekana Kwamba Alikuwa na Ndoto Ya Kumiliki Kampuni Ya Ndege Tangu Yuko Shule Ya Sekondari Lakini Kutokana na Sera Mbovu za Kiuchumi za Serikali Ya Awamu Ya Kwanza Ndoto Yake Ilichelewa Kidogo. Lakini Kwa Kuwa Alikuwa na Dhamira Yenye Nguvu Sana Ndani Yake Ndoto Yake Iliendelea Kuwa Hai Kwa Miaka Mingi Ndani Yake. Mwaka 1993 Akiwa na Umri wa Miaka 50 Aliweza Kuileta Ndoto Yake Katika Uhalisia Kwa Kuanzisha Kampuni Ya Usafiri wa Anga Ya Precision Air, Mwanzoni Ikifanya Kazi Ya Kubeba Watalii.

– Mwaka 2011 Kampuni Ya Usafiri wa Anga Ya Precision Air Ilisajiliwa Kwenye Soko La Hisa La Dar es Salaam (DSE) Kama Kampuni Ya Umma Kwa Kila Mtu Kununua Umiliki na Kunufaika na Faida. Michael Shirima Mwenyewe Aliendelea Kubakia Kuwa Mmiliki Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi Ya Wakurugenzi Huku Akienza Sehemu Kubwa Ya Hisa za Kampuni Pia Kwa Kampuni Ya Kenya Airways Ya Kenya. Licha Ya Changamoto za Kiuchumi, Udhaifu wa Kisiasa na Majanga Kama Ugonjwa wa Covid19 Kampuni Ya Precision Air Imeendelea Kuwa Imara Kwenye Biashara Ya Anga Bila Utendaji Wake Kuyumba.

– Michael Shirima ni Mmoja Kati Ya Watu Wanaostahili Heshima Kubwa Sana Kwenye Nchi Hii Kwa Mapinduzi Makubwa Waliyoleta Kwenye Sekta Binafsi Baada Ya Kuvumilia Sera Mbovu Za Mrengo wa Kushoto Zilizodhoofisha Sana Biashara na Uchumi Kwa Ujumla Kwa Miongo Kadhaa. Huyu ni Mmoja Kati Ya Mashujaa Muhimu Wasiozungumziwa (Unsung Hero).

– Mwaka 2016 Gazeti la Forbes Africa Lilimtaja Michael Ngaleku Shirima Kama Tajiri Namba 6 Tanzania, Akitajirika Zaidi Kupitia Ukuaji wa Kampuni Ya Precision Air Baada Ya Hisa Zake Kupanda Sana Thamani na Sehemu Kubwa Kununuliwa na Kampuni Ya Kenya Airways. Eneo Lingine Lililomtajirisha ni Uwekezaji Mkubwa Katika Beni Ya I & M Pamoja na Vyanzo Vingine Mbalimbali Vya Kipato.

– Michael Shirima Pia Ndiye Mwanzilishi wa Kituo Cha Watoto Yatima Kinachoitwa “Cornel Ngaleku Children Centre” Kilichopo Katika Kijiji cha Leto, Usseri, Rombo.

– Akiwa ni Mjasiriamali Mwenye Mafanikio Makubwa Michael Ngaleku Shirima Aliyezaliwa Katika Kijiji cha Ngaseni, Usseri, Rombo Amekuwa Mmoja Kati Ya Wachagga Walioiheshimisha Sana Jamii Ya Wachagga na Kilimanjaro Kwa Mambo Makuu Waliyofanya Kwenye Maisha Yao.

– Leo Amehitimisha Safari Yake Ya Maisha Akiwa na Umri wa Miaka 80.

– RIP LEGEND, The Great Son of Kilimanjaro.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *