KUGUNDULIKA KWA MADINI YA “LITHIUM” KILIMANJARO.

– Kampuni ya Kimarekani inayojulikana kama Titan Lithium Inc. imeweza kugundua uwepo wa madini ya Lithium katika eneo la upande wa kusini wa Kilimanjaro. Upande wa kusini wa mlima Kilimanjaro ndio upande yanapoanzia makazi ya wachagga kuelekea kwenye tambarare ambazo kwa sehemu kubwa ni mashamba ya wachagga yanayoendelea kubadilika kwa kasi kuwa mji.

– Katika taarifa hii ambayo imesambaa sana kwenye habari siku chache zilizopita licha ya kueleza kwamba maeneo hayo mawili waliyogundua madini hayo ya Lithium na kuyaita Titan 1 na Titan 2 yana ukubwa wa kilomita za mraba 200 hawajaeleza yako katika vijiji gani exactly. Eneo la mita za mraba 200 ni eneo kubwa ambalo linaweza kuwa limejumuisha mpaka vijiji vitatu mpaka vitano au zaidi ambapo shughuli za uchimbaji wa madini haya ni lazima utakuja na usumbufu mkubwa kwa wakazi wa maeneo husika.

– Nimejaribu kufuatilia habari hii kwa kina sana kuweza kufahamu haya maeneo kamili lakini habari yenyewe imezungumzwa kwa ujumla sana kuhusu maeneo husika kuweza kuyaelewa kwa usahihi.

– Madini ya lithium ni kati ya madini ambayo yako katika uhitaji mkubwa duniani kwa sasa na hasa huko mbele tunakoelekea kwa ni madini yanayotumika katika kutengeneza betri mbalimbali na hasa betri za magari ya umeme ambayo ni teknolojia ya magari inayokuwa kwa kasi sana duniani. Kwa sababu ya kujali sana mazingira na tafiti kuonyesha kwamba nishati ya mafuta huenda ikapotea kabisa duniani miaka kadhaa ijayo, mbadala wake umekuwa ni mitambo na magari ya umeme ambayo yanaendeshwa kwa betri zinazochajiwa.

– Kuonyesha kwamba eneo hili la teknolojia ya nishati ya umeme kutumika katika magari limekuwa sana ni kwamba hata tajiri namba 1 duniani kwa sasa “Elon Musk” sehemu kubwa ya utajiri wake unatokana na biashara ya kuuza hisa za kampuni yake ya magari ya umeme ya “Tesla” ambayo yako katika viwango bora sana kwa sasa tofauti na zamani. Hivyo kugundulika kwa madini ya lithium ni habari njema sana kwa kampuni zote za magari ambazo zinaelekea kugeukia moja kwa moja katika uzalishaji wa magari ya umeme pekee miaka michache ijayo. Kampuni nyingi zina mpango wa kuachana kabisa na gari za injini zinazoendeshwa na mafuta na kuhamia kwenye magari ya umeme.

– Hata hivyo licha ya baadhi ya watu kuwa na mtazamo chanya lakini kutokana na namna sera za nchi zilivyo na mifumo ya nchi ilivyokaa hakuna matumaini makubwa kwamba Kilimanjaro na watu wake watafaidika moja kwa moja na ugunduzi wa madini. Kama ilivyokuwa kwa mikoa mingine yenye madini mengi mbalimbali sera na sheria za madini zitabaki kuwa ni zile zile na hata kama kuna faida yoyote itakayopatikana itapelekwa hazina na kugawanywa kama inavyofanyika kwa mapato yanayotokana na utalii wa mlima Kilimanjaro ambayo ni makubwa sana pia. Hili angalau lingewezekana kuwa na utaratibu tofauti kama kungekuwa na serikali za majimbo kutegemea pia na namna sera na sheria zingekuwa zimewekwa.

– Kama kuna mtu mwenye kujua maeneo haya mawili ambayo yanasemekana kwamba madini haya ya Lithium yamegundulika ambayo yana ukubwa wa takriban kilomita za mraba 200 atusaidie vijiji husika.

– Karibu kwa maoni.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *