UKOO WA MOSHA.

– Mosha ni ukoo mkubwa, mashuhuri, maarufu na mkongwe sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Huu ni ukoo uliosambaa katika maeneo ya vijiji vingi vya Uchaggani, Kilimanjaro kuanzia maeneo ya katikati kuelekea mashariki. Ukoo wa Mosha ni ukoo wa watu wengi mashuhuri wanaofanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania. Wachagga wa ukoo wa Mosha pia wanasemekana ni watu wenye hulka ya ujasiri, ubabe na wenye kutamani mambo makubwa sana.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Mosha unasemekana kuwa ulikuwa ni ukoo uliokuwa unatawala katika kijiji cha Mkyashi, Kilema pamoja na kijiji cha Rosho, Kilema kwa kiasi na hata kijiji cha Ruwa, Kilema kwa kiasi na ndio ulikuwa ukoo wenye nguvu zaidi Kilema mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1700. Baadaye Ngowi na mtoto wake Mremi walipokuja Kilema na kuimarisha utawala wa umangi wenye nguvu zaidi inasemekana kwamba koo zote ziliutambua na kukaa chini ya utawala huo isipokuwa ukoo wa Mosha ambao waligoma kukaa chini yake.

– Wachagga wa ukoo wa Mosha huko Kilema wanasemekana kwamba hata mifugo yao haikuchangamana na mifugo ya utawala, waligoma kulipa kodi kwa utawala na hata wachagga wa kwa Mosha hawakuoana na familia ya wamangi hususana katika miaka ya mwanzoni ya utawala huo ambao walikuwa wameugomea na hata wao ni kama walikuwa wamejitenga na jamii nzima. Hata hivyo baadaye baada ya utawala wa umangi kupata nguvu zaidi na uhasama baina yao na ukoo Mosha na hata koo nyingine kupungua, wachagga wa ukoo wa Mosha walianza kuingilia na utawala wa umangi na hata kuanza kulipa kodi ili kufaida mambo mengine kama ulinzi, ardhi kubwa zaidi na nzuri na hata upendeleo mwingine kutoka kwenye serikali ya umangi.

– Kutoka kwenye historia tena katika himaya ya umangi Kirua Vunjo kwenye miaka ya 1770’s kulikuwa na mtawala aliyeitwa Mangi Mosha. Mangi Mosha wa Kirua Vunjo alitawala himaya ya Kirua Vunjo katika miaka ambayo himaya ya umangi Kilema inatawaliwa na Mangi Kombo, baba yake na Mangi Rongoma. Katika wakati huo Kilema chini ya Mangi Kombo ilikuwa imevamiwa na Marangu ambayo ilikuwa inatawaliwa na Mangi Ngarawiti. Mangi Ngarawiti wa Marangu na majeshi yake pamoja na washirika wake kutoka Rombo waliwashambulia Kilema ambapo Kilema walilazimika kukimbilia uhamishoni Kirua Vunjo kwa Mangi Mosha ili kuwa salama dhidi ya majeshi ya Marangu na washirika wao.

– Inasemekana kwamba Mangi Kombo alikuwa na mke mrembo sana aliyeitwa Malyandu ambaye Mangi Mosha alimtamani na kujaribu kumshawishi awe mke wake kitu kilichopelekea Malyandu kukasirika na kurudi Kilema kwa hasira bila kujali kwamba anaweza kuuawa yeye na mtoto wake na majeshi ya Marangu. Kwa ufupi ni kwamba baadaye siri hiyo ilikuja kujulikana na kupelekea ugomvi mkubwa kati ya Kilema na Kirua Vunjo. Hadhithi hii na nyingine kama hizi zimeelezwa kwa kina zaidi kwenye kitabu cha “Miaka 700 ya Wachagga”.

– Hivyo ukoo wa Mosha kutoka Mkyashi Kilema na Kirua Vunjo uliendelea kusambaa na kupatikana katika maeneo mengine mengi ya Uchagga kama inavyoelezwa.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kiwalaa, Mbokomu.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Tella, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Marua, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kanango, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kwamare, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Pofo, Kilema.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ngangu, Kilema.

– Ukoo wa Mosha unapatikana katika kijiji cha Marawe Kyura, Kilema.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Ruwa, Kilema.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Makami Chini, Kilema.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa uchache katika kijiji cha Rauya, Marangu.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa uchache katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa uchache katika kijiji cha Sembeti, Marangu.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ashira, Marangu.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mshiri, Marangu.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyala, Marangu.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa uchache katika kijiji cha Komalyangoe, Marangu.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kiraracha, Marangu.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kitowo, Marangu.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kotela, Mamba.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Mosha unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mamsera Kati, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Mosha wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mengeni chini, Keni, Rombo.

Tunahitaji mchango zaidi wa mawazo juu ya ukoo wa Mosha ili kuongeza maudhui zaidi ya ukoo huu na koo za wachagga kwa ujumla katika kujenga ardhi zaidi ya kufuatilia historia na maendeleo sambamba na kutunza historia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mosha.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mosha?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mosha?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mosha?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mosha una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mosha wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mosha kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mosha?

9. Wanawake wa ukoo wa Mosha huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mosha?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mosha?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mosha?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mosha kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *