Ahsanteni Urithi Wetu Wachagga

Habari Wafuasi wa Urithi Wetu Wachagga.

Nachukua Fursa Hii Kuwashukuru Wote Ambao Tumekuwa Pamoja Hapa Kwa Kipindi cha Miezi Miwili Mkifuatana na Sisi Katika Mfululizo wa Makala za Historia Ya Wachagga kwa Kipindi cha Miaka 700 Kadiri Tulivyojaliwa Kukusanya Taarifa.

Napenda Niwashukuru Wote Waliofuatilia Mwanzo Mpaka Mwisho Kwani Nyinyi Ndio Sababu Tumeweza Kuweka Mfululizo Huu wa Makala Hizi za Historia Kwa Kipindi cha Miezi Miwili Mfululizo Bila Kuruka Hata Siku Moja, Kama Jinsi Tulivyokuwa Tumepanga. Kwa Hilo Tumefanikisha kwa 100%.

Lakini Kipekee Kabisa Niwashukuru Zaidi Wale Ambao Walitoa Mchango Wao wa Mawazo Kupitia Comments Kwa Namna Moja au Nyingine, Wameongeza Sana Thamani na Ufafanuzi Zaidi wa Kazi Hii.

Nawashukuru sana Pia Wale Waliopiga Simu na Wengine Kufika Inbox na Tumeweza Kupata Nyongeza na Mapendekezo Zaidi Ambayo Tutaenda Kuyafanyia Kazi Katika Kuboresha Zaidi Kazi Hii Ya Huu wa Historia.

Kwa Wale Ambao Wanasubiri Kitabu Nawaomba Wavute Subiri Kwani Hakitachukua Muda Mrefu Tena Kwani Sasa Tunakamilisha Maboresho Machache Kutokana na Michango Ya Mawazo na Vyanzo vya Taarifa Vya Wadau Mbalimbali na Kurekebisha Mapungufu Kidogo Yaliyokuwepo Ili Kuhakikisha Tunakuwa na Kazi Iliyo Bora Zaidi Inayoenda Kusomwa na Kizazi cha Leo Iweze Kuwa Sehemu Ya Mabadiliko na Fikra Sahihi Zaidi za Watu Wetu.

Karibu kwa Mchango Wowote wa Mawazo wa Ziada Juu Ya Mradi Huu na Endapo Kuna Mtu Ana Maoni Yoyote, Kero, Malalamiko, au Anahisi Kwamba Kuna Jambo Lolote Halikwenda Sawa, Labda Uonevu au Upendeleo wa Eneo au Mtu Yeyote Pia Unakaribishwa.

Tunaahidi Kwamba Tutafanyia Kazi Jambo Lolote Lenye Maslahi Kwa Wachagga Litakalowekwa Hapa Kupitia Kazi Hii.

Mambo Mazuri na Makubwa Zaidi Yako Njiani, Bado Tutaendelea Kuwa Pamoja Sana.Ahsanteni.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *