UKOO WA ASSEY

– Asei ni ukoo mkongwe sana wa wachagga unaopatikana kwa wingi zaidi katika maeneo ya vijiji vya himaya za Kirua Vunjo na Kilema. Kutoka kwenye historia ukoo wa Asei unaonekana kuwa chimbuko lake ni katika himaya ya umangi Kirua Vunjo.

– Kutoka katika historia ya utawala wa umangi Kirua Vunjo Asei anaonekana kuwa ni kizazi cha nne kutoka kwa mtawala wa mwanzoni kabisa anayefahamika kwa jina la Msanya. Asei akiwa ni mjukuu wa Kesi, mtoto wa Msanga na baba yake Mangi Pakula.

– Huyu anasemekana kupitia simulizi za mdomo za zamani maarufu kama “oral traditions” kwamba alitawala theluthi moja ya himaya ya Kirua Vunjo kwenye kipindi cha mwishoni mwa miaka ya 1600 au mwanzoni mwa miaka ya 1700.

– Ukoo wa Asei uliendelea kusambaa katika maeneo ya vijiji vingine vya jirani na vijiji cha mbali zaidi pia, hivyo:-

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Yamu, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Manu, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kileuo, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mero, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Legho, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Pofo, Kilema.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ruwa, KIlema.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu.

– Ukoo wa Asei unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kimbogho, Mamba.

Kuna mambo mengi sana hayajulikani kuhusu ukoo wa Asei hususan kama ni tawi la zamani sana kutokea kwenye ukoo wa Kesi na namna ulivyosambaa na kuenea. Tunahitaji kupata taarifa zaidi kuhusu ukoo huu mkongwe sana wa wachagga ili kuweza kuongeza katika maudhui ya ukoo na koo za wachagga kwa ujumla ili kujenga uelewa na hamasa kwa kizazi cha sasa na vijavyo katika kuendelea kujifahamu na kuhamasika kufanya makubwa katika maisha.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Asei.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Asei?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Asei?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Asei?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Asei una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Asei wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Asei kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Asei?

9. Wanawake wa ukoo wa Asei huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Asei?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Asei?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Asei?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Asei kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *