UKOO WA KOMBE.

– Kombe ni ukoo maarufu wa wachagga wanaopatikana kuanzia upande wa magharibi ya Kilimanjaro na wengine katikati kuelekea mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Kombe ni ukoo wenye wengi mashuhuri wanaofanya vizuri katika fani mbalimbali kama taaluma, ujasirimali, biashara, kwenye mashirika, ndani ya taasisi, serikalini na mashirika binafsi ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Kutoka kwenye historia Kombe katika upande wa magharibi wa Kilimanjaro ndani ya himaya ya umangi Machame alikuwa ni mtoto wa Mangi Kiwaria(Kivaria) ambaye alitawala Machame katika miaka ya mwanzoni ya 1700. Kombe mtoto wa Kiwaria anasemekana katika utawala wake hakufanikiwa kupata mtoto wa kiume hivyo kupoteza matumaini ya kupata mrithi katika kiti cha utawala. Hata baadaye alikuja kufanikiwa kupata watoto wa wawili wa kiume na kumrithisha yule mkubwa kiti cha umangi.

– Hata hivyo wachagga wa ukoo wa Kombe ndani ya Machame waliotokea kwenye tawi hilo wamekuwa ni wachache sana na badala yake ukoo wa Kombe umesambaa kwa wingi zaidi katika eneo la Vunjo. Lakini pamoja na hayo bado haiko wazi kabisa kama ukoo huu wa Kombe unauopatikana zaidi katika eneo la Vunjo unahusiana moja kwa moja na Kombe kutokea Machame. Ukoo wa Kombe uliosambaa katika vijiji vingi mbalimbali katika mashariki ya kati ya Uchagga ni ukoo mkubwa wenye watu wengi na wenye umashuhuri mkubwa.

– Ukoo wa Kombe umeendelea kukua na kusambaa sana na unapatikana kwa wingi na kwa uchache katika vijiji mbalimbali mashariki ya kiti ya Uchagga, Kilimanjaro na wengine wakipatikana kwa kiasi upande wa magharibi kabisa ya Uchagga, Kilimanjaro.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lawate, Siha/Sanya Juu.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Wari, Machame.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mero, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Ngangu, Kilema.

– Ukoo wa Kombe unapatikaa kwa uchache sana katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Komela, Marangu.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Lyasomboro.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kotela, Mamba.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Komakundi, Mamba.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiria, Mamba.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Lole Marera, Mwika.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Lole, Mwika.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uuwo, Mwika.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirimeni, Mwika.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

– Ukoo wa Kombe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mengwe chini, Mengwe, Rombo.

Bado kuna taarifa nyingi hazifahamiki kuhusiana na ukoo wa Kombe na namna ulivyosambaa katika vijiji vya Uchagga kuanzia mashariki mpaka magharibi. Sasa ili kupata maudhui mengi zaidi juu ya ukoo tunahitaji kupata taarifa zaidi zitakazosaidia kuongeza mchango mkubwa kwenye tafiti zinazoendelea na pia kujenga hamasa kwa wanaukoo na wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kombe.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kombe?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kombe?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kombe?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kombe una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kombe wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kombe kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kombe?

9. Wanawake wa ukoo wa Kombe huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kombe?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kombe?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kombe?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kombe kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

 1. Kombe wote uchagani (siyo Kombo) asili yao ni moja, Machame. Labda ningeshauri ukae na wazee wa ukoo huo uko Mashariki ya Uchagani wakuelezee vizuri. Wengi wao wataweza kukuhesabia hata vizazi vilivyotokea Machame katika nusu ya pili ya karne ya 19. Sababu kubwa ikiwa ni changamoto za kisiasa zilizokuwa zikiongezeka kule Machame katika kipindi hicho, hasa ukichukulia kuwa Kombe kwa asili ulikuwa ni ukoo wa kiutawala Machame (royal family).

  Kombe uliyemzungumzia hapa ni Kombe II, aliyepewa jina la babu yake, Kombe I ambaye ndiye aliyemzaa Mangi Kiwaria.

  Baba yake na Kombe I ndiye aliyeanzisha himaya na dola ya Machame, katikati ya karne ya 16 ikiwemo kuiweka mipaka ya himaya hiyo.

  Uzao wa Kombe I ndiyo umekuwa ukoo wa kifalme Machame uliotoa koo maarufu kama vile Mushi (wa Machame) na Shangali.

  Kiasili, shina la ukoo huu ni Machame Foo, na inasemekana hata kufikia mwanzoni kabisa mwa karne ya 20, wazee wa ukoo huu walikuwa wakienda kutambikia Foo pamoja na Sienyi, karibu na mtu Kikafu.

  Sijawahi kusikia kama wana masharti ya vyakula, lakini kulikuwa na mila ya kwamba hawakutumia maji yaliyotokana na mto uliopo Nkuu. Pia kulikuwa kuna mila kwamba ni mtoto wa kwanza tu wa kiume kwa mama ndiye aliyeweza kurithishwa kiti cha utawala.

  Wengine pia nao wanaweza kuongezea hapa kuhusiana na ukoo huu wa Kombe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *