UKOO WA MASSAWE.

– Ukoo wa Massawe ni ukoo mkongwe sana na unaweza kuwa ndio ukoo maarufu kuliko zote Uchaggani. Lakini ukoo wa Massawe pia ndio ukoo unaopatikana maeneo mengi na vijiji vingi uchaggani pengine kuliko zote. Kwanza sio rahisi kukuta eneo la uchagga Kilimanjaro lisilo na ukoo wa Massawe kabisa japo kuna maeneo ambayo ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi kuliko maeneo mengine. Hili limepelekea wakati mwingine hata mchagga wa kawaida nje ya Kilimanjaro asiyetokea ukoo wa Massawe kuitwa Massawe kwa kuwa ni mchagga.

– Kutoka kwenye historia matawi ya ukoo wa Massawe yamekuwa yakipatikana maeneo mbalimbali ya Uchagga japo tawi kuu la asili bado ni vigumu kuweza kuwa na uhakika nalo. Hata hivyo licha ya kwamba ukoo wa Massawe unapatikana kila mahali uchaggani lakini unapatikana kwa wingi zaidi katika himaya umangi Kibosho na katika himaya za Rombo.

– Kutoka kwenye tafiti za kihistoria inafahamika kwamba ukoo wa Massawe ni kati ya koo tatu kongwe sana Kibosho sambamba na Msele na Kulaya. Asili ya ukoo huu wa Massawe ndani ya Kibosho unasemekana kuwa ni katika kijiji cha Maua na Otaruni ambapo makazi ya mwanzoni zaidi ya ukoo wa Massawe yanasemekana kuwepo kwa wingi au ukongwe wa vizazi vya ukoo huu unavyoweza kupatikana hususan Massawe wa tawi la Otaru.

– Tawi lingine la ukoo wa Massawe ndani ya Kibosho ambalo ni kongwe sana ni tawi la ukoo wa Massawe katika kijiji cha Umbwe, Kibosho. Tawi hili la ukoo wa Massawe ya Massawe-Mbishi katika kijiji cha Umbwe, Kibosho lina kumbukumbu ya vizazi mpaka wakati wa Mbishi ambapo Mzee aliyekuwa hai mpaka katikati ya karne ya 20 au zaidi anayekumbukwa na historia ni Mzee Rafael Massawe. Huyu ndiye amekuwa chanzo cha jina la eneo maarufu Umbwe, Kibosho kama “Kwa Rafael”, kwani ndiye aliyetokana na kizazi hiki cha tawi hili la ukoo wa Massawe.

– Hata hivyo matawi ya ukoo wa Massawe ni mengi sana na hivyo vizazi vyake vimetanuka sana kiasi kwamba hata ni vigumu kujua lini tawi hilo liligawanyika. Kwa Kibosho peke yake kuna zaidi ya matawi 25 ya ukoo wa Massawe ambayo yana vizazi vinavyokwenda mpaka karne ya 18 au 17 ukiacha matawi mapya ambayo yanaweza kuwa yameanzishwa karne ya 19, 20 na hata 21. Hapo hujazungumzia matawi mengine ya maeneo mengine kama vile upande wa magharibi huko Machame, katikati ya Uchagga na mashariki huko Rombo.

– Tawi lingine la ukoo wa Massawe ambalo ni maarufu ni katika himaya ya umangi Mkuu, Rombo ndilo ambalo lilikuja kuwa kizazi cha watawala kuanzia Mzee wa zamani zaidi wa karne ya 18 au mwishoni mwa karne ya 17 aliyeitwa Soya. Kizazi hicho cha Massawe wa Mkuu, Rombo ambapo wakati wa mwanzoni wa Mzee wa ukoo aliyeitwa Soya hawakuwa watawala lakini baadaye walikuja kuingia kwenye mstari wa watawala kwa vizazi vya mbeleni. Mangi Kinabo ambaye ni mtoto wa Mature na mjukuu wa Kimbarika alikuwa ni kati ya watawala mashuhuri na wenye nguvu sana Kilimanjaro karne ya 19 kutokea kwenye kizazi hiki ambapo sasa Kimbarika mwenyewe babu wa Kinabo ni mtoto wa Kiriri na mjukuu wa Soya.

– Ukoo wa Massawe ni ukoo wenye watu wengi sana hivyo unaonekana kuwa ulikuwa ni ukoo wa watu walioamua kutawanya matawi yao karibu kila eneo la Uchagga kwa sababu mbalimbali na matawi hayo yakaendelea kugawanyika sana. Ni ukoo wa watu makini na wanaofanya vizuri sana maeneo mbalimbali. Hata hivyo licha ya ukoo wa Massawe kuwa maarufu sana pengine kuliko ukoo mwingine wowote lakini bado kwa mujibu wa takwimu za google sio ukoo unaoongoza kwa idadi kubwa ya watu Uchaggani.

– Wachagga wa Ukoo wa Massawe wanapatikana kuanzia magharibi katika himaya ya umangi Siha/Sanya Juu katika vijiji vya Lawate na Sanya Juu.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa kiasi Masama magharibi katika kijiji cha Sufi.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Saawe, Masama.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana katika kijiji cha Ngira na Sonu, Masama.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shari/Uraa na Kyeeri, Machame.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi kidogo katika kijiji cha Uswaa, Machame.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Wari Sinde eneo la Kalali na Urara Machame.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Nronga Machame.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi katika huko Lyamungo, Machame.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Umbwe na Kifuni, Kibosho.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kindi, Kibosho.

– Ukoo wa Massawe wanapatika kwa wingi katika kijiji cha Manushi, Kibosho hususan Manushi Ndoo.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana pia katika vijiji vya kata ya Okaoni, Kibosho.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Uri, Kibosho.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Maua, Kibosho.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Otaruni Kibosho.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uchau na Mloe, Kibosho.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi sana katika vijiji vya Kirima Juu, Kirima Kati na Boro, Kibosho.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi katika maeneo ya himaya ya umangi Uru.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa kiasi maeneo ya Mbokomu, Old Moshi.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Tela, Old Moshi.

– Ukoo wa Massawe kwa kiasi katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Massawe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Massawe unapatikana kwa kiasi kwenye baadhi ya vijiji vya Kilema.

– Ukoo wa Massawe unapatikana kwa kiasi Marangu katika kijiji cha Mbahe na kijiji cha Lyasongoro.

– Ukoo wa Massawe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kotela, Mamba.

– Ukoo wa Massawe unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kotela, Mamba.

– Ukoo wa Massawe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Komakundi, Mamba.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa kiasi katika maeneo ya Maring’a, Kimangaro na Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana huko Ugweno.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi sana katika maeneo ya Keni, Rombo.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi sana katika eneo la Mkuu, Makiidi na Mokala, Rombo.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi sana pia katika eneo la Mashati, Msaranga na Kisale, Rombo.

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi sana pia katika vijiji vya Usseri Rombo kama vile Kingachi, Ngaseni, Kirongo n.k.,

– Ukoo wa Massawe wanapatikana kwa wingi pia katika vijiji mbalimbali vya Tarakea, Rombo.

Tunahitaji msaada wa taarifa zaidi juu ya ukoo huu mashuhuri sana wa Massawe popote pale zinapoweza kupatikana.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Massawe?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Massawe?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Massawe?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Massawe una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Massawe wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Massawe kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Massawe?

7. Wanawake wa ukoo wa Massawe huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa ukoo wa Massawe?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Massawe?

Karibu kwa Maoni na Maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *