UKOO WA MBUYA.

– Ukoo wa Mbuya ni ukoo mkubwa unaopatikana zaidi katika eneo la katikati ya Kilimanjaro. Yaani ukoo wa Mbuya umesambaa katika eneo kubwa la uchagga la katikati lakini haupatikani sana magharibi ya mbali wala mashariki ya mbali.

– Wachagga wa ukoo wa Mbuya wamekuwa ni watu wenye kujituma na wapenda maendeleo na inafahamika kwamba msomi mhandisi wa kwanza Tanganyika alitokea ukoo wa Mbuya ambaye aliitwa Eng. Ainamensa Mbuya kutokea katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi aliyepata shahada yake ya kwanza ya uhandisi huko London, Uingereza.

– Kutoka kwenye historia tunaona pia kwamba ukoo wa Mbuya ulikuwa ni ukoo wa watu mashuhuri na ndio ukoo uliokuwa unatawala katika eneo lote la Kyou na Maua huko Kilema. Ukoo wa Mbuya ulikuwa ni ukoo wenye nguvu na uliweza kutawala eneo hili ndani ya Kilema mpaka kufikia mwishoni mwa karne ya 17 au mwanzoni mwa karne ya 18 kabla ya mfululizo wa utawala wa umangi ulioitawala Kilema yote na kudumu mpaka katikati ya karne ya 20.

– Ukoo wa Mbuya unapatikana kwa kiasi kwenye vijiji kadhaa katika eneo la himaya ya umangi Uru.

– Ukoo wa Mbuya unapatikana pia kwa kiasi katika vijiji kadhaa katika himaya ya umangi Old Moshi.

– Ukoo wa Mbuya unapatikana pia maeneo mbalimbali ya Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mbuya unapatikana kwa wingi katika vijiji vya Rosho, Kyou/Maua na Ruwa.

– Ukoo wa Mbuya unapatikana kwa kiasi katika baadhi ya vijiji vya Marangu.

– Ukoo wa Mbuya unapatikana kwa kiasi katika baadhi ya vijiji vya Mamba.

– Ukoo wa Mbuya unapatikana kwa wingi pia katika baadhi ya vijiji vya Mwika.

Bado kuna taarifa chache sana kuhusiana na makazi zaidi na asili ya ukoo wa Mbuya huko Uchaggani. Tunahitaji mchango wa mawazo kuhusu taarifa zaidi juu ya ukoo huu mkongwe na uliokuwa mashuhuri sana wa wachagga wa Mbuya.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mbuya?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mbuya?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mbuya?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mbuya una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Mbuya wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mbuya kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mbuya?

7. Wanawake wa ukoo wa Mbuya huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mbuya?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mbuya?

Karibu kwa Maoni na Maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *