SIKU KUU YA WACHAGGA, “CHAGGA DAY”, “MFIRI-OU-WACHAKKA”

.Leo Tarehe 10/Novemba Ni Siku Kuu Ya Wachagga Ambayo Ilikuwa Inasherehekewa Zamani Kabla Ya Uhuru wa Tanganyika na Miaka Michache Baada Ya Uhuru wa Tanganyika Kama Siku Ambayo Ilikuwa Ni Muhimu Sana Kwa Wachagga Ndani na Nje Ya Kilimanjaro.

Ni Siku Kuu Ambayo Ilikuwa Kubwa Sana Kilimanjaro na Kwa Wachagga Waliokuwa Wanaishi Maeneo Mengine Nje Ya Kilimanjaro, Miaka Ya 1950’s Mpaka 1960’s Kuliko Hata Siku Kuu Ya Christmas.

Matukio Ya Siku Kuu Ya Wachagga Yaliyokuwa Yakichapishwa na Gazeti La Wachagga La “Komkya” Lililokuwa Linasambazwa Maeneo Mbalimbali Ndani na Nje Ya Kilimanjaro Hususan Kwenye Miji Ya Mombasa, Nairobi na Dar es Salaam Yalizidi Kuinogesha Siku Kuu Ya Wachagga na Kuifanya Ya Kipekee Sana.

Ni Siku Ambayo Wachagga Walikuwa Wanasherehekea Siku Ambayo Walifikia Mafanikio Ya Juu Kabisa Kiutawala Ambapo Walifanikiwa Kuwa na Kiongozi Mkuu wa Serikali Ya Wachagga Ambaye ni Mangi Mkuu, Aliyekuwa Pia Mwenyekiti wa Baraza La Halmashauri Kuu Ya Wachagga(Chagga Supreme Council).

Hili Tutaendelea Kuliona Zaidi Hili Kwenye Historia.

Siku Kuu Hii Ya Wachagga Ambayo Ilikuwa ni Siku Ya Mapumziko Kilimanjaro Ilikuwa ni Sehemu Ya Kauli Mbiu Ya Kuhimiza Maendeleo Ya Kilimanjaro Chini Ya Utawala wa Mangi Mkuu Iliyokuwa Ikisindikizwa na Wimbo Maalum wa Taifa La Wachagga Kilimanjaro Uliojulikana Kama “Ikumi Lya Novemba Nyi Mfiri-Ou-Wachakka”.

Wimbo Huu Pia Ulikuwa Ukiimbwa Katika Shule Zote Kilimanjaro Kuanzia Magharibu Mpaka Mashariki.Sherehe za Siku Kuu Ya Wachagga Zilikuwa Ni Sherehe Kubwa Zilizosherehekewa Kuanzia Kwenye Ngazi Ya Vijiji na Maeneo Ya Umangi Mpaka Kwenye Ikulu Ya Mangi Mkuu Moshi Mjini.

Sherehe Hii Iliambatana na Michezo Mbalimbali, Maonyesho na Matukio Mengine Yaliyoipamba Sana Siku Hii Sambamba na Hotuba Mbalimbali Za Kuhamasisha Ari Ya Maendeleo na Mapambano Makubwa Zaidi Ya Kiuchumi Kilimanjaro.

Niwatakie Wachagga Wote Heri Ya Siku Hii Muhimu Kwa Wachagga Ambayo Iliweza Kuongezea Utukufu Mkubwa Zaidi na Ufahari Kwa Jamii Ya Wachagga Kilimanjaro na Niwakaribishe Tuendelee Kujifunza Mambo Mengi Zaidi Kuhusu Sisi Wenyewe.

Unaweza Kuchagua Mchagga Mmoja Utakayemtumia Ujumbe Huu na Kuiboresha Siku Yake Kwa Kumtakia Heri Ya Siku Hii Muhimu Kwetu Kwa Ujumbe Huu:-

“(Heri Ya Siku Kuu Ya Wachagga Kwako ……………, Siku Hii Muhimu na Ya Kipekee Kwa Wachagga Ikakuongezee Imani na Matumaini Zaidi Katika Yale Yote Unayoazimia Kuyafanikisha Kama Ambavyo Imekuwa Desturi Tangu Enzi Za Wakale Wetu)”. “(Happy Chagga’s Day To You ………….., May This Special and Unique Day For The Chagga People Give You Faith and Hope To Attain Your Life Goals As It Has Been A Custom Since The Times of Our Ancestors).

Heri Ya Siku Kuu Ya Wachagga Kwenu Wote.

Kwa Wale Wenye Kuweza Kusherehekea Kwa Namna Yoyote Ile Niwatakie Maazimisho Mema wa Siku Kuu Ya Wachagga.

Ahsanteni Sana.

Aikenyi Kishari.

You may also like...

Popular Posts

3 Comments

  1. kimaroprize@gmail.com says:

    Ni yapi mavazi ya asili ya wachaga.na je taifa hili liliishia wapi Hadi kua chini ya Tanganyika na je mipakaya Kilimanjaro ya Leo ndio Ndio himaya ya wachaga..je wameru ni wachaga?

    1. Karibu sana.

      Yote hayo tumeelezea kwenye kitabu cha Miaka 700 Ya Wachagga.

    2. Mipaka ya Kilimanjaro ni eneo lote la mkoa wa Kilimanjaro kwa sasa ukiondoa maeneo ya Upareni.

      Ndio Wameru ni wachagga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *