MIAKA 700 YA WACHAGGA.

Miaka 700 Ya Wachagga Ni Mfululizo wa Baadhi Ya Makala Za Historia Ya Wachagga Kwa Wastani wa Kipindi Cha Miaka 700 Kwa Kadiri Tulivyojaliwa Kukusanya Taarifa Kutoka Kwenye Vyanzo Mbalimbali.

Ni Kazi Iliyochukua Muda Mrefu na Kuhusisha Kusoma Vitabu Vingi, Kudadisi, Kutafiti, Kutafakari na Kujadili Matukio Mbalimbali Ya Kihistoria Kuhusu Kilimanjaro na Wachagga. Watu Mbalimbali Pamoja na Taasisi Zimechangia Katika Kuwezesha Kazi Hii Kufanikiwa Kwa Mchango Wao wa Hali na Mali Walioutoa Wakati wa Utafiti.

Kipekee Kabisa Nimshukuru Mjomba Wangu Paul Mlinga Aliyeko Kule Massachussets, Marekani Kwa Msaada Mkubwa Alioutoa Katika Kusaidia Kupatikana Kwa Vitabu na Makala Nyingi Sana Zilizowezesha Kusaidia Kupatikana Kwa Taarifa Nyingi Muhimu Zilizokuwa Zinakosekana.

Pili Nimshukuru Kaka Yangu Steve Steven Rameses Sharra, Aliyeko Hapa Moshi Kwa Kuongeza “Challenge” na Kusaidia Kupatikana Kwa Taarifa Nyingi za Msingi Hasa Mwanzoni Sambamba na Kusaidia Kupatikana Kwa Vyanzo Vingine Zaidi Vya Taarifa. Shukran Nyingine za Kipekee Ziende Kwa Kanisa Katoliki, Jimbo Katoliki Moshi Hasa Katika Parokia Ya Kristo Mfalme na Parokia Ya Mbokomu Chini Ya Shirika La “Holy Ghost Fathers” Hususan Sista Aquina.

Natoa Shukran Pia Kwa Kanisa La Kilutheri Usharika wa Moshi Mjini.

Niishukuru Pia Taasisi Ya “Wanamaendeleo Moshi” Kwa Imani, Uvumilivu na “Support” Yao Tangu Mwanzo Kabisa wa Wazo Hili, Sambamba na Kilimanjaro Development Forum(KDF) Kwa Mchango Wao Mkubwa Katika Hatua za Mwanzoni Hususan Diwani Mstaafu Michael Kilawila.

Tumepata Ushirikiano Mkubwa Sana Kila Eneo Tulilotembelea Kilimanjaro na Tumekutana na Watu Wengi Sana Ambao Siwezi Kuwataja Hapa Wote Lakini Wamechangia Kufanikisha Hili Kwa Namna Nyingi.

Ushirikiano Pia Tuliopata Kutoka Kwenye Maktaba Mbalimbali Kama Maktaba Ya Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MOCU), Maktaba Ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Maktaba Ya Mkoa Kilimanjaro, Maktaba Ya Mkoa Arusha, Maktaba Ya Taifa Dar es Salaam, Maktaba Ya Makumbusho Ya Taifa Dar es Salaam, Maktaba Ya Shule Ya Msingi Mshiri, Marangu n.k., Zimekuwa Sehemu Muhimu Sana Katika Kufanikisha Mchakato Huu.

Siwezi Kusahau Pia Mchango Tulioupata Kutoka Kwa Maofisa Mbalimbali wa KNCU Hususan Dada Dora Nkya Ambaye Ndiye Alishughulika Kuhakikisha Kila Kinachohitajika Kinapatikana.

Watu Wengine Muhimu Waliosaidia Kutoa Mchango wa Mawazo na Vyanzo Muhimu Vya Taarifa Ni Pamoja na Prof. Temu, Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr. Swai wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Pamoja na Prof. Ngowi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi Ya Dar es Salaam.

Mwisho na Kipekee Kabisa Nimshukuru Mzee Wangu Abisai Temba Kwa Msaada wa Vitabu Vyake Pamoja na Mjadala Mzito Ambao Ulisaidia Kufungua Fursa Zaidi za Kujifunza.

Mwisho Kabisa Niwashukuru Wachagga Wote na Watanzania Kwa Ujumla Kwa Kuwa Ni Kwa Sababu Yenu, Ndio Maana Tumeweza Kufanya Kazi Hii, Bila Uwepo Wenu Isingefanyika.

Nitakuwa Naweka Makala Baadhi Hapa Kwenye Ukurasa wa Facebook wa Akaunti Hii Lakini Niombe Sana Kwamba Ni Kwa Ajili Ya Followers wa Hapa Facebook Peke Yake, Ni Kosa Kusambaza Sehemu Nyingine Yoyote. Ikiwa Kuna Mtu Unataka Ajifunze Basi Mwalike Aje Kusoma Hapa. Na Kama Hayupo Facebook Basi Asubiri Maboresho na Maandilizi Ya Historia Iliyopangiliwa Kwa Usahihi na Inayoonyesha Vitu Vingi na Ufafanuzi Uliyoboreshwa Zaidi Kwa Mfumo wa Kitabu.

Baada Ya Makala Hizi za Historia Utafuata Mfululizo wa Makala Nyingine Nyingi Nzuri na Za Kusisimua Sana Zinazotoa Ufafanuzi wa Mambo Mbalimbali Ya Wachagga Ambazo Tutaweka Hapa na Kwenye Website Ya “Urithi Wetu Wachagga”, Na Ambapo Itakuwa Ni Ruksa Kuzisambaza Popote Unapotaka.

Ahsanteni sana.

Aikenyi Kishari.

Urithi Wetu Wachagga.

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *