TUNAHITAJI KUWA “SERIOUS” ZAIDI KATIKA HILI AU KUNA SHERIA ZINAZOTUBANA?

– Wakati Mwingine Kutojua Historia na Kutojihangaisha Kufuatilia Mambo Yanayowahusu Huwa Ni Chanzo cha Jamii Kujisahau Sana.

Hivi Tunajua Kwamba Ni Njia Ya Marangu Pekee Katika Kupanda Mlima Kilimanjaro Ambayo Ina Hotels(Huts) za Kufikia?

Njia Nyingine Kupanda Mlima Kilimanjaro Unapaswa Kupanda na Mahema Ya Kubeba. Lakini Ajabu Zaidi Ni Kwamba Hizo Huts Zenyewe Zilizopo Njia Ya Marangu Zilijengwa Miaka Ya 1910’s na Mfanyabiashara Mkulima Mkubwa wa Kijerumani Aliyeitwa Dr. Emil Theodor Foster.

Dr. Forster Alihamia Kilimanjaro Mwaka 1908 Iliyokuwa Chini Ya Wajerumani na Aliishi Old Moshi, Wakati Huo Ikiwa Ndio Makao Makuu Ya Wajerumani Kilimanjaro. Dr. Forster Ndiye Alijenga “Kibo Hotel” Iliyopo Pale Marangu, Arisi na “Old Moshi Hotel” Ambayo Haijulikani Hata Ilipo.

Dr. Forster Ndiye Alijenga Hizo “Lodge” Za Kupumzikia Watalii Wakiwa Wanapanda Mlima Ambazo Aliziita Bismarck, Peters na Johannes na Ndiye Aliyeanzisha Taasisi Inayoshughulika na Safari za Kupanda Mlima Kilimanjaro Iliyoitwa, “Kilimanjaro Mountaineering Association”.

Baadaye Ndipo Zilikuja Kubadilishwa Majina Wakati wa Waingereza na Kuitwa “Mandara Hut”, “Horombo Hut” na “Kibo Hut”, Lakini Hakuna Mabadiliko Makubwa.

Mwaka 1920 Baada Wajerumani Kushindwa Vita Ya Kwanza Ya Dunia na Kunyang’anywa Makoloni Yao, Serikali Ya Waingereza Ilitaifisha Mali za Dr. Forster na Kuzitaji Kama Mali za Adui Hivyo Hoteli Zake na Hizi Lodge Zikachukiliwa na Serikali Ya Uingereza na Yeye Mwenyewe Dr. Forster Kuondolewa Kilimanjaro Akaelekea Amerika Ya Kusini.

Dr. Forster Ambaye Pia Alikuwa ni Baba Mkwe wa Dr. Bruno Guttman, Alikuwa Pia Ndiye Mlezi(Mentor) wa Joseph Merinyo Maro, Mtoto wa Jenerali Merinyo Maro wa Old Moshi Ambaye Pia Alikuwa Ndiye Mwanzilishi na Rais wa Chama cha Wakulima Wazawa cha Kilimanjaro Native Planters Association (K.N.P.A) Alichoanzisha Mwaka 1924, Kilichokuja Kupata Nguvu Sana na Mafanikio Makubwa na Kupelekea Kuvunjwa na Joseph Merinyo Kuondolewa Kwa Sababu za Kisiasa Mwaka 1930.

Kuvunjwa Kwa K.N.P.A Ndio Kulipelekea Kuanzishwa Kwa KNCU Mwaka 1932.Baada Ya Uhuru wa Tanganyika Serikali Ya Uingereza Ilikabidhi Kila Kitu Kwa Serikali Ya Tanganyika.

Lakini Mpaka Leo Ni Zaidi Ya Miaka 100 Hakuna Vibanda(Huts) Nyingine Zilizojengwa.Je Kuna Sheria Zinazozuia?Nini Maoni Yako?

MANDARA HUT.
HOROMBO HUT.
MANDARA HUT.
MANDARA HUT.
HOROMBO HUT.
HOROMBO HUT.
KIBO HUT.
KIBO HUT.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *