UKOO WA MTEI.

– Mtei ni ukoo maarufu wa wachagga unaopatikana katika ukanda wa mashariki ya kati na kwa wingi zaidi katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu makini na wengine mashuhuri sana wanaofanya vizuri sana na waliofanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali hususan katika taaluma, ujasiriamali na biashara.

– Ukoo wa Mtei umekuwa na umaarufu wa kuwa na watu wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa ambao wameacha alama na majina makubwa maeneo mbalimbali. Kwa hapa Moshi mjini tunaweza kuona hata eneo la Majengo Kwa Mtei ni eneo limepata umaarufu kwa umashuhuri wa Mzee Mtei wa eneo hilo aliyepata kuishi hapo miaka mingi iliyopita.

– Moja kati ya watu muhimu, maarufu na mashuhuri sana katika historia ya nchi ya Tanzania aliyepata kuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania ametokea kwenye ukoo huu wa Mtei, Edwin Mbiliewu Mtei. Huyu alipata pia kuwa waziri wa fedha, katibu mkuu wa Jumuiya ya zamani ya Afrika mashariki kabla haijavunjika na kufanya kazi pia kwenye taasisi za fedha za kimataifa. Edwin Mtei pia ndiye mwanzilishi na Mwenyekiti wa kwanza wa chama maarufu cha siasa na chenye ufuasi mkubwa Tanzania Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kilichokuja na itikadi za mrengo wa kulia wa kisiasa na kinachosimamia sera mbadala baada ya zile za mwanzoni za mrengo wa kushoto kushindwa vibaya.

– Ukoo wa Mtei umesambaa zaidi kwenye baadhi ya vijiji vya upande wa mashariki ya Uchagga kuanzia mashariki ya kati mpaka mashariki ya mbali unapopatikana kwa uchache kwenye baadhi ya vijiji na kwa wingi kwenye vijiji vingine.

– Hivyo ukoo wa Mtei unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Arisi, Marangu.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mengwe chini, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Manda Juu, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shimbi Kati, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Shimbi Mashariki, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Makiidi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Maharo, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mokala, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa wingi kiasi katika vitongoji vya Kata ya Kelamfua, Mkuu Mjini, Rombo.

– Ukoo wa Mtei unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ikuini, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.

Pamoja na kwamba ukoo wa Mtei umetoa watu wengi mashuhuri lakini bado kuna uhaba mkubwa wa taarifa juu ya ukoo huu wenye ngome upande wa mashariki ya Uchagga, Kilimanjaro. Tunahitaji kupata taarifa zaidi kuhusiana na ukoo wa Mtei ili kuongeza maudhui zaidi kwenye maktaba ya ukoo wa Mtei na jamii ya wachagga kwa ujumla. Maudhui haya yana lengo la kusaidia katika kujenga hamasa na mshikamano mkubwa zaidi kuanzia ngazi ya familia, ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla kwa kizazi cha sasa na vinavyoendelea kuja miaka ijayo katika kupigania tamaduni, historia na maendeleo makubwa na endelevu kwa jamii ya wachagga.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mtei.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mtei?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mtei?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mtei?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mtei una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mtei wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mtei kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mtei?

9. Wanawake wa ukoo wa Mtei huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mtei?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mtei?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mtei?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mtei kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *