UKOO WA KAVISHE.

– Kavishe ni ukoo mkubwa wa wachagga unaopatikana kwa wingi sana katikati ya eneo la mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Kavishe ni ukoo mkubwa na wenye watu wengi mashuhuri wanaofanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali hususan kwenye biashara na ujasiriamali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Kavishe unasemekana kwamba walikuwa ndio watawala wa iliyokuwa himaya ndogo ya umangi Ushiri iliyopo upande wa mashariki wa eneo la Mkuu, Rombo kabla ya kuvuka mto Ungwasi ambayo leo hii inajumuishi kata ya Ushiri/Ikuini na vijiji vya Ubaa, Ushiri na Ikuini. Inafahamika kwamba mpaka kufikia mwishoni mwa karne ya 19 katika miaka ya 1890’s Ushiri kama ilivyokuwa Shimbi ilikuwa ni himaya huru inayojitegemea na iliyowahi kuwa na nguvu sana kihistoria.

– Katika muongo huu wa karne ya 19 himaya hii ya umangi Ushiri ilikuwa inatawaliwa na Mangi Melani kutoka kwenye ukoo wa Kavishe na ndipo ilivamiwa na Mangi Kinabo wa Mkuu akishirikiana na majemedari wake mashuhuri wa kivita Mlatie Mrema na Mtarania Mtei wakaiweka chini ya utawala wa Mkuu. Ushiri na watu wake iliyokuwa inatawaliwa na Mangi Melani wa ukoo wa Kavishe walijisalimisha na kukaa chini ya utawala wa Mkuu iliyokuwa ikitawaliwa na Mangi Kinabo.

– Hivyo ukoo wa Kavishe uliendelea kukua na kusambaa katika vijiji mbalimbali vya ukandaa huu wa mashariki ya mbalimbali ya Uchagga kwa wingi na kwa uchache kwenye baadhi ya vijiji.

– Hivyo ukoo wa Kavishe unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mahango, Mahida, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Nguduni, Mahida, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mamsera Kati, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Mengwe Juu, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Megwe Chini, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mengeni Chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Aleni Chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shimbi Masho, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Shimbi Kati, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Shimbi Mashariki, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ibukoni, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Makiidi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mokala, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa wingi kiasi katika vitongoji cha Kata ya Kelamfua, Mkuu Mjini, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ubaa, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ikuini, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kirua, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kiraeni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Katangara, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mrere, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kisale, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mahorosha, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Msaranga, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Kavishe unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kitowo, Olele, Rombo.

Tunaomba mchango zaidi wa mawazo juu ya ukoo wa Kavishe katika kuongeza maudhui zaidi ya ukoo huu. Taarifa zaidi zitazidi kufungua fursa za utafiti zaidi na kuongeza maudhui zaidi ya ukoo wa Kavishe kwa faida ya jamii ya wachagga kujitambua zaidi na kujenga hamasa na mshikamano zaidi kuelekea katika mafanikio makubwa.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kavishe.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kavishe?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kavishe?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kavishe?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kavishe una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kavishe wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kavishe kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kavishe?

9. Wanawake wa ukoo wa Kavishe huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kavishe?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kavishe?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kavishe?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kavishe kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *