UKOO WA KIWELU.

– Kiwelu ni ukoo wa kichagga ambao unapatikana kwa kiasi katika vijiji kadhaa vya maeneo ya katikati ya Uchaggani, Kilimanjaro. Licha ya kutokuwa ukoo uliosambaa sana lakini ni ukoo ulioweza kutoa watu kadhaa mashuhuri katika nchi hii wakiwemo wafanyabiashara na wanasiasa maarufu. Moja kati ya watu mashuhuri wanaofahamika sana kutokea kwenye ukoo huu ni aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshi mjini kwa muda mrefu Mzee Philemon Ndesamburo Kiwelu anayetokea katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi. Pia watu wa familia yake wameendelea kufanya vizuri katika kisiasa.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Kiwelu umekuwa ni ukoo muhimu katika masuala ya utawala katika maeneo wanayopatikana kwani wamekuwa ni wanajeshi imara na hodari sana. Pia ukoo wa Kiwelu umekuwa umetokea kutoa wachili na watu wengine wenye ushawishi katika siasa za Uchaggani. Moja kati ya mabogadi wa Mangi Meli ambao walinyongwa pamoja naye ni Sindato Kiwelu aliyekuwa mtu wake wa karibu sana na wa sana na Mangi Meli. Huyu Sindato Kiwelu aliyekuwa mtu wa karibu sana wa Mangi Meli na ambaye alinyongwa pamoja naye ndiye babu wa baba yake Mzee Philemon Ndesamburo.

– Ukoo wa Kiwelu umekuwa ni ukoo wa watu wanaofanya vizuri sana katika maisha katika nyanja mbalimbali na wanaopatikana ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania.

– Kutokana na ukoo huu kukua na kusambaa maeneo mbalimbali ya Uchaggani, kilimanjaro ukoo wa Kiwelu unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Kiwelu wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Kiwelu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kotela, Mamba.

– Ukoo wa Kiwelu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo wa Kiwelu unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Mboni, Mamba.

– Ukoo wa Kiwelu unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

Ukoo wa Kiwelu bado ni miongoni mwa koo ambazo historia yake imejificha sana hivyo tunahitaji kupata taarifa zaidi juu ya ukoo huu ambao umeacha alama kubwa katika historia ya wachagga, Kilimanjaro. Upatikanaji wa taarifa zaidi kuhusu ukoo mkongwe wa Kiwelu utasaidia sana katika shughuli za utafiti na zaidi kuongeza maudhui ya ukoo huu na koo za wachagga kwa ujumla katika kuwajengea ari na hamasa zaidi wachagga wa ukoo huu katika kufanikisha mambo makubwa katika ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye ukoo, ngazi ya ukoo mzima na ngazi ya jamii ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kiwelu.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kiwelu?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kiwelu?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kiwleu?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kiwleu una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kiwelu wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kiwelu kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kiwelu?

9. Wanawake wa ukoo wa Kiwelu huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kiwelu?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kiwelu?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kiwelu?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kiwelu kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *