UKOO WA MROSSO.

– Mrosso ni ukoo mkubwa, mashuhuri na maarufu sana wa wachagga unaopatikana kwa zaidi upande wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo uliosambaa katika maeneo ya vijiji vingi sana vya mashariki ya Uchagga kwa wingi kwenye baadhi ya vijiji na kwa uchache kwenye vijiji vingine.

– Wachagga wa ukoo wa Mrosso wengi ni wafanyabiashara na wajasiriamali waliosambaa katika maeneo mengi ya ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. Kutoka kwenye historia hakuna mengi sana tuliweza kupata ya kimaandishi kuhusu ukoo wa Mrosso lakini kutoka kwenye simulizi za wachagga wa ukoo huu na koo za jirani ni kwamba ukoo wa Mrosso ni ukoo wa watu wajasiri sana na wajasiriamali wazuri sana.

– Ukoo Mrosso umesambaa na unapatikana kuanzia maeneo ya mwishoni mwa ukanda wa mwa mashariki ya kati ya Uchagga kwa uchache katika baadhi ya vijiji na kwa wingi zaidi katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga kwenye vijiji vingi na kwa wingi sana.

– Hivyo, ukoo wa Mrosso unapatikana kuanzia katika kijiji cha Lyasomboro, Marangu.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mshiri, Marangu.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mawanjeni, Mwika.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mahango, Mahida, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kidondoni, Challa, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mengwe Juu, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mengwe chini, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Manda Chini, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mengeni chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Aleni chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shimbi Masho, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shimbi Mashami, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Shimbi Kati, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Shimbi Mashariki, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Maharo, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Makiidi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mokala, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa kiasi katika vitongoji vya kata ya Kelamfua, Mkuu Mjini, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ushiri, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Ikuini, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kiraeni, Kirwa/Keni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Keni, Kirwa/Keni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kirua, KirwaKeni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mrere, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Katangara, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kisale, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahorosha, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Msaranga, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kooti, Olele, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kitowo, Olele, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kirongo chini, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kingachi, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kwalakamu, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ubetu, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Ngaseni, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Leto, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ture, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Urauri, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Nessae, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Msangai, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kibaoni, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Nayeme, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mbomai, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Mrosso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kikelelwa, Tarakea, Rombo.

Hatujafanikiwa kupata maandiko yanayozungumzia ukoo wa Mrosso wala taarifa rasmi zaidi ya kuuliza taarifa nyingi za mdomoni hivyo bado kuna mengi yasiyofahamika kuhusiana na ukoo wa Mrosso. Tunahitaji mchango wa mawazo kuhusiana na ukoo huu mkubwa na maarufu wa Mrosso unapatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Taarifa hizi ni muhimu katika kuongezea kwenye tafiti za koo zinazoendelea sambamba na kusaidia kuongeza maudhui zaidi katika maktaba ya ukoo wa Mrosso na maktaba ya wachagga kwa ujumla. Taarifa hizi zitasaidia pia katika kujenga hamasa na mshikamano kwa kizazi cha sasa na vinavyokuja katika kulinda jamii, tamaduni zake na kuyaendea mafanikio makubwa.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mrosso.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mrosso?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mrosso?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mrosso?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mrosso una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mrosso wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mrosso kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mrosso?

9. Wanawake wa ukoo wa Mrosso huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mrosso?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mrosso?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mrosso?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mrosso kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *