KWA NINI KILIMANJARO NI MUHIMU SANA KWA WACHAGGA?

KWA NINI KILIMANJARO NI MUHIMU SANA KWA WACHAGGA?

KWA NINI ARDHI YA WACHAGGA HAIUZIKI?

KWA NINI WACHAGGA HUENDA NYUMBANI KUSHEREHEKEA KILA MWISHO WA MWAKA?

KWA NINI MCHAGGA AKIFARIKI NI LAZIMA AKAZIKWE KWENYE ARDHI YA KILIMANJARO?

Watu Wengi Ikiwemo Baadhi Yetu Sisi Wachagga Hawana Majibu Ya Uhakika Kwa Maswali Haya Ambayo Ni Muhimu Sana Kwa Kila Mchagga Kujiuliza.

Linapo Kuja Suala La Ardhi Ya Kilimanjaro Kwa Wachagga Basi Ni Sawa na Kuitaja Miji Ya Maka na Madina Kwa Waislamu au Kuitaja Yerusalemu Kwa Wakristo.

Kilimanjaro ni Ardhi Takatifu Ambayo Wazee Wetu wa Kichagga Waliiweka Wakfu Rasmi Karne Nyingi Sana Zilizopita Kwamba Mchagga Yeyote Ana Mahusiano Ya Karibu Sana na Ardhi Aliyorithishwa na Wazee Wake Kutokea Vizazi na Vizazi.

Tafiti za Kihistoria Zinaonyesha Kwamba Huu Utamaduni Haukuanzia Kwa Wachagga Baada Ya Kuhamia Kilimanjaro Rasmi Kuanzia Takriban Miaka 700 Iliyopita, Tafiti Zinaonyesha Kwamba Ni Utamaduni wa Wachagga Tangu Huko Ethiopia Ya Kaskazini Ambapo Tamaduni Nyingi za Asili za Wachagga Zimeanzia.

Kutoka Kwenye Tafiti za Kihistoria Waandishi Kadhaa Waligusia Jambo Hili Kuanzia Nathaniel Mtui, Dr. Bruno Guttman na Hata Sir Charles Dundas Kwamba Wachagga Ni Watu Ambao Wamekuwa na Uzalendo Mkubwa na Ardhi Yao Tangu Kale na Kale Kuliko Jamii Nyingi Duniani. Na Jambo Hili Limeendelea Kuwa Dhahiri Mpaka Leo Hii Karne Ya 21, Kwani Kwa Sehemu Kubwa Bado Ardhi Ya Urithi Ya Mchagga Hauiziki na Mchagga Mara Kwa Mara Hurudi Katika Ardhi Yake Angalau Mara Moja Kwa Mwaka. Lakini Pia Mchagga Yeyote na Vizazi Vyake Vyote Baada Ya Maisha Ya Hapa Duniani Hurudi Kupumzishwa Katika Ardhi Yake Ya Milele, Ardhi Takatifu Ya Urithi Kilimanjaro.

Ni Imani Ya Mchagga Tangu Kale na Kale Kwamba Ardhi Yake Takatifu Ya Urithi Ya Kilimanjaro Aliyorithishwa Kutoka Vizazi na Vizazi Ndio Nyumbani Kwake, Ndio Mwanzo Mpaka Mwisho wa Maisha Yake Ya Hapa Duniani na Hawezi Kukaa Mbali na Ardhi Hii Takatifu Sana Kwake Kwa Muda Mrefu Sana na Ndio Maana Mara Kwa Mara Hurudi Nyumbani Ikiwa Anaishi Miji Ya Mbali Angalau Mara Moja Kila Mwaka.

Thamani Hii Kubwa Sana Ambayo Wazee wa Zamani wa Uchagga Waliipa Ardhi Yao Takatifu Ya Kilimanjaro Illiwafanya Wachagga Kuwa na Uzalendo Mkubwa Zaidi Kwa Nchi Yao Takatifu Ya Kilimanjaro Kuliko Jamii Nyingine za Kiafrika.

Na Hata Mpaka Wachagga wa Leo Hii Karne Ya 21 Kwa Kiasi Kikubwa Sana Bado Tumeendelea Kuonyesha Uzalendo wa Hali Ya Juu Sana Kwa Thamani Kubwa Ambayo Tumeendelea Kuipa Ardhi Takatifu Ya Urithi Ya Kilimanjaro Kutoka Kwa Wazee Wetu na Kuendelea na Msimamo Kwamba Hauiziki na Daima Itabaki Kuwa ni Nyumbani.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *