UKOO WA RINGO.

– Ringo au zamani ulikuwa ukiitwa pia Iringo ni ukoo mkongwe sana wa kichagga unaopatikana katika maeneo kadhaa ya vijiji vya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Ringo wengi ni wapambanaji sana wakiwa wamesambaa maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania wakifanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali. Mmoja kati ya watu maarufu kutoka kwenye ukoo huu wa Ringo ni mwanadada rubani anayesemekana kuwa ndiye mwanamke wa kwanza mtanzania kurusha ndege aina ya Boeing anayejulikana kwa jina la Hilda Wendy Ringo.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Ringo au kama ilivyokuwa inajulikana zamani pia kama Irinngo kwa uchaggani inasemekana ngome yao kuu ilikuwa ni katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi. Ukiwa ni mmoja kati ya koo kubwa sana za eneo la katikati ya Old Moshi ukoo wa Ringo unasemekana walikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi na kama watawala wa kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Ringo ulitoa watu majasiri na imara sana katika moja kati ya majeshi yaliyoweza kufanikisha mambo makubwa sana Kilimanjaro na eneo la Afrika mashariki kwa ujumla kama vikosi vya majeshi ya Mangi Rindi Mandara na Mangi Meli Mandara vilivyoweza kutawala maeneo makubwa na hata kuwashinda vita wajerumani. Wachagga wa ukoo wa Ringo wameendelea kufanya vizuri na katika maeneo mengi na wengi kupiga hatua kubwa.

– Ukoo wa Ringo umeendelea kusambaa zaidi katika maeneo ya vijiji vingine vya Uchagga na hata himaya nyingine za Uchagga nje ya Old Moshi. Ukoo wa Ringo pia umeendelea kuongezeka sana idadi ya watu na unaendelea kukua zaidi na kupatikana kwa wingi zaidi na katika vijiji zaidi vya Uchagga, Kilimanjaro.

– Hivyo ukoo wa Ringo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Ringo unapatikana kwa wingi pia katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Ringo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Ukoo wa Ringo unapatikana kwa wingi pia katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Ringo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Ringo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Ringo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ruwa, Kilema.

– Ukoo wa Ringo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Ringo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.

– Ukoo wa Ringo wanapatikana kwa uchache sana baadhi ya vijiji Rombo.

Tunahitaji mchango zaidi wa mawazo juu ya ukoo wa Ringo na maeneo zaidi unakopatikana ili kuongeza maudhui ya ukoo huu na koo za wachagga kwa ujumla. Bado tuna kuna taarifa chache sana juu ya ukoo wa Ringo ambao ni mkongwe sana Uchaggani.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Ringo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Ringo?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Ringo?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Ringo?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Ringo una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Ringo wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Ringo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Ringo?

9. Wanawake wa ukoo wa Ringo huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Ringo?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Ringo?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Ringo?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Ringo kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *