TUNAELEKEA WAPI KAMA JAMII?

Wakati wowote katika historia, swali moja ambalo watu au jamii hupaswa kujiuliza ni tunaelekea wapi? Hili ni swali muhimu sana kwa sababu linasaidia kuwapa watu/jamii fursa na nafasi ya kuamua kwa usahihi kule wanakotaka kuelekea badala ya kusubiri hatma iamue yenyewe. Kwa sababu watu wakishindwa kuamua wanaelekea wapi watajikuta sehemu ambayo hawakutamani kufika na kujilaumu tena kwa kushindwa kupanga kwa usahihi.

Rais mashuhuri sana wa Marekani aliyekuwa Rais wa 16 wa nchi hiyo kwa jina Abraham Lincoln (1809 – 1865) amewahi kusema haya, “the best way to predict the future is to create it”. Ikimaanisha “Namna bora zaidi ya kutabiri kule unakoelekea ni kupaumba”. Msemo huo huo ulikuja kurudiwa tena baadaye na mbobezi mashuhuri wa sayansi ya usimamizi wa mashirika/makampuni duniani mwenye asili ya Ujerumani aliyehamia Marekani Peter Druker (1909 – 2005).

Lakini swali la tunaelekea wapi ni swali gumu sana kujibu na kupanga kwa usahihi ikiwa hatujui tumetokea wapi. Ni muhimu sana watu kufahamu kwa usahihi kabisa juu ya kule walikotokea ili kuweza kuamua kwa usahihi zaidi kule wanakoazimia kwenda ili kufika sehemu watakayojivunia kufika kwa wakati sahihi.

Hata hivyo suala la kufahamu kule tulikotoka ili tuweze kupanga kwa usahihi kule tunakokwenda ni jukumu letu sote kwani inapaswa wote tufahamu kwa usahihi tulikotoka ili tujue tunachagua jambo gani kwa pamoja. Haya ni maarifa yanayopaswa kusomwa na watu rika zote wa jamii husika kuanzia vijana wadogo wanaokua mpaka wazee watu wazima kabisa. Hili ni jukumu letu sisi sote ambao tuna matamanio ya kuona uelekeo wa jamii yetu unaenda kwa namna chanya au kwa namna ambayo tunataka wenyewe.

Wakati tukiwa tunaendelea kupanga mikakati ya kule tunakoazimia kufika tuendelee kujielimisha kwa maarifa ya kitabu maalum cha kule tulikotoka mpaka hapa tulipofika ili tunapoendelea kupanga mipango ya mbeleni iwe rahisi kuelewana na kuamua kwa usahihi. Uelewa huu mpana na sahihi juu ya kule tulikotoka utasaidia hata kuepuka kurubuniwa na kuhadaika na maneno ya watu wa kuja ambao wanatumia maneno ya kutujengea hatia tunapojaribu kujenga umoja na mshikamano ili kututoa kwenye lengo na kuhakikisha hatupigi hatua kubwa kuwazidi wao.

Ni muhimu zaidi kuhakikisha kwamba tunaacha urithi sahihi kwa vizazi vinavyofuata na kuacha mipango bora endelevu ya jamii ambayo vizazi vinavyofuata vitajivunia sana.

Kwa sasa tuko kwenye awamu ya pili ya mauzo ya kitabu hiki ambayo inaelekea kumazilika kwa nakala zilizopo hivyo tunahimiza zaidi ambao bado hawajapata nakala zao wachukue hatua haraka. Tunafurahi na kujivunia kwamba kwa sasa sio wachagga pekee wameonyesha kuvutiwa na kununua nakala za kitabu hiki bali hata watu wa makabila mengine hususan Wahaya wameonyesha kuvutiwa sana na kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga”, na tayari wameanza kununua pia. Hivyo injili hii ya wachagga imeendelea kusambaaa mpaka kwa watu wa jamii nyingine hususan Wahaya.

Kuna wale wachagga ambao wana watoto wao waliozaliwa nje ya nchi na kuishi huko, hivyo wanashindwa kusoma kitabu hiki ambacho kiko kwa lugha ya kiswahili na kupendekeza kuwe na tolea lingine la kitabu kwa lugha ya kiingereza. Tumeendelea kuwajulisha kwamba tolea la kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” kwa lugha ya kiingereza kwa faida ya wachagga waliozaliwa na kuishi nje ya nchi linaendelea kufanyiwa kazi na mpaka Juni 2023 litakuwa limetoka.

Hili linakwenda sambamba na kuhakikisha kwamba matoleo yote mawili ya kitabu, “Miaka 700 Ya Wachagga” kwa lugha za kiswahili na kiingereza yanapatikana Amazon. com ili kupeleka injili hii ya wachagga kwenye majukwaa ya kimataifa.

Maudhui haya yakipatikana kwa wingi zaidi kwenye majukwaa sahihi ya kimataifa kama alivyojitahidi pia kuandika Dr. Bruno Guttman yatasaidia kuongeza umaarufu wa jamii yetu kimataifa. Kwa sababu mara nyingi tumekuwa tukisoma vitabu mbalimbali vinavyoandikwa na waandishi mashuhuri duniani kama wakina Robert Greene na kukutana na mifano mingi ya tawala za Ulaya, Amerika, Asia na kwa Afrika tunaona mfano wa tawala mbalimbali za Ethiopia ambayo imekuwa ikiandikwa tangu miaka zaidi ya 2,500 iliyopita ikitumika sana kwa sababu maudhui ya kuhusu tawala zao yanapatikana kwa wingi kwenye majukwaa ya kimataifa.

Lakini wachagga tuna fasihi kubwa sana iliyoandikwa, na kwa hapa Afrika mashariki tumezidiwa labda na Ethiopia yenyewe. Sasa ni jukumu letu kuhakikisha kwamba maudhui yetu yanaenda kwenye majukwaa ya kimataifa ili kuongeza umashuhuri wa jamii yetu kimataifa na kutuletea faida nyingi mbalimbali hususan utalii wa kitamaduni na kihistoria.

Kwa sababu ni watu wajinga pekee ndio huwa hawajui kwamba umaarufu na umashuhuri wa mtu, watu au jamii hutokana na kusambaa kwa wingi kwa hadithi yake au yao. Kama huna umaarufu au umashuhuri ni kwa sababu hadithi yako haijatengenezwa kwa namna ya kuvutia na kusisimua na kusambazwa kwa wingi katika majukwaaa mbalimbali duniani. Hakuna kingine cha zaida ya hapo.

Habari njema kwa watu wa Moshi ni kwamba kwa sasa nakala za kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” kwa awamu ya pili ambayo inaelekea kumalizika vinapatikana pale “Lutheran Uhuru Hotel and Conference Centre” Shanti Town. Unaweza kuwasiliana na Brother Nelson Munisi kwa simu na +255 754 068 852.

Kwa Dar es Salaam kitabu kinapatikana maeneo ya Mbezi Beach, Massana au unaweza kuwasiliana na wanaofanya usambazaji wakakufikishia popote. Unaweza kuwasiliana na Juhudi Kessy +255 788 433 968.

Kwa miji na mikoa mingine yote pia nakala za kitabu zinatumwa kila mahali ndani na nje ya Tanzania. Wasiliana na Deodath Kimario +255 755 932 022.

Karibu tuendelee kurudisha utukufu uliopotea.

Karibu kwa Maoni au Maswali.

Urithi Wetu Wachagga.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *