UKOO WA KIMAMBO.

– Ukoo wa Kimambo ni ukoo mkubwa na mkongwe sana wa wachagga uliobeba sehemu muhimu ya historia ya wachagga, Kilimanjaro. Katika Kilimanjaro makazi ya asili na ya mwanzoni kabisa ya wachagga wa ukoo wa Kimambo ni katika kijiji cha Mowo, Old Moshi. Hiki ni kijiji kikongwe sana na kilichobeba historia ya kipekee kwani hata jina la mji “Moshi” linatambuliwa na historia ya wachagga kwamba lilianzia katika kijiji hiki kwa ushawishi wa ukoo wa Kimambo.

– Kutoka kwenye historia inasemekana kwamba makazi ya ukoo wa Kimambo yalianzia katika ukanda wa juu wa msituni katika kijiji cha Mowo, Old Moshi kabla ya baadaye kuhamia katika eneo la “Kimochi” katika kijiji cha Mowo ambapo baadaye lilikuja kuwa ni soko kubwa na moja kati ya masoko makubwa na makongwe katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Inafahamika kwamba ukoo wa Kimambo walikuwa ni wachagga mahodari katika taaluma ya kutengeneza mifereji au tunaweza kusema ni mainjinia wa kutengeneza mifereji maarufu kama “furrow surveyors”.

– Licha ya kwamba taaluma hii ya kutengeneza mifereji ni teknolojia ya juu sana ambayo wachagga waliondoka nayo kutoka kwenye bonde la mto “Nile” huko maeneo ya Misri na kuja nayo Kilimanjaro lakini moja kati ya wazee wa mwanzoni kabisa wa ukoo wa Kimambo waliokuwa mahiri sana katika uhandisi wa mifereji aliitwa Musoko. Mzee wa Musoko wa ukoo wa Kimambo na vizazi vya kabla yake na baada yake walifanya kazi kubw aya kurithisha taaluma hii ya kipekee kwa wachagga wa ukoo wa Kimambo wa vizazi vilivyofuatia.

– Ukoo wa Kimambo ndio ukoo uliokuwa unatawala na uliokuwa na nguvu zaidi katika vijiji vya upande wa magharibi wa Old Moshi vya Mowo, Sango na Shia. Ni katika utawala wa Mangi Ndetia aliyetawala himaya ya umangi Old Moshi kabla ya Mangi Salia ndipo ukanda huu wa vijiji vya upande wa magharibi ya Old Moshi viliwekwa chini ya utawala Mangi kutokea Tsudunyi aliyetawala Old Moshi yote. Kabla ya hapo ukoo wa Kimambo ulikuwa ndio wenye nguvu na watawala katika ukanda huu wa vijiji vya upande wa magharibi ya Old Moshi.

– Ukoo wa Kimambo uliendelea kusambaa katika maeneo ya vijiji vingine vya Old Moshi kwa wingi na kwa kiasi katika maeneo mengine ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga mashuhuri wengi wameendelea kutokea kwenye ukoo huu wa Kimambo katika nyakati mbalimbali za historia ya wachagga mpaka sasa huku ukoo huu ukiendelea kupatikana katika maeneo mengi.

– Ukoo wa Kimambo unapatikana kwa kiasi katika baadhi ya maeneo ya vijiji vya Kibosho.

– Ukoo wa Kimambo unapatikana kwa kiasi katika baadhi ya maeneo ya vijiji vya Uru.

– Ukoo wa Kimambo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Fukeni, Kata ya Mbokomu, Old Moshi.

– Ukoo wa Kimambo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kimamboni, kata ya Mbokomu, Old Moshi.

– Ukoo wa Kimambo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

– Ukoo wa Kimambo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Kimambo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Kimambo unapatikana kwa kiasi katika baadhi ya maeneo ya Kirua Vunjo.

Tunahitaji taarifa zaidi kuhusiana na ukoo huu mkongwe wa Kimambo wenye historia ya kipekee uchaggani hivyo tunaomba mchango zaidi wa mawazo juu ya ukoo huu.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kimambo?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kimambo?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kimambo?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kimambo una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Kimambo wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kimambo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kimambo?

7. Wanawake wa ukoo wa Kimambo huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kimambo?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kimambo?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

1 Comment

  1. Famous:
    +Prof. Kimambo

    + Dr Kimambo

    + famous Entrepreneur William Kimambo, RIP wa pale Kiborlon Mochi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *