THE GREAT WALL OF KIBOSHO, “UKUTA MKUBWA WA KIBOSHO”.

THE GREAT WALL OF KIBOSHO, “UKUTA MKUBWA WA KIBOSHO”

– Pichani Inaonyesha Magofu Ya Iliyokuwa Ngome Kubwa Na Imara Sana Iliyojengwa na Mangi Sina Mushi, Kibosho Miaka Ya 1870’s.

– Magofu Haya Yapo Katika Kijiji Cha Mkoring’a, KNCU Ya Juu, Kibosho, Karibu na Stendi Ya Daladala za Moshi – Kibosho Kirima.

– Ukuta Mkubwa Uliozunguka Ngome Hii Ulikuwa na Urefu wa Wastani wa Mita 3 Kwenda Juu na Mita 2 Kuingia Chini Ardhini na Upana wa Mita 2. Ukubwa wa Ngome Hii Ilikuwa Ni Kama Viwanja 15 Vya Mpira na Mzunguko wa Huu Ukuta Ulikuwa Ni Karibu Kilomita 2.

– Yaani Ni Kusema Ngome Ya Kibosho Ilikuwa Ni Kubwa Zaidi Ya Mara Kumi Ya Ngome Kongwe Ya Zanzibar, Pale Forodhani.

– Ndani Ya Ngome Hii Kulikuwa Na Nyumba Zaidi Ya 100 Za Kichagga, Kulikuwa na Nyumba za Ghorofa Kubwa Mbili na Ghala Kubwa La Kuhifadhia Silaha, Soko Kubwa na Maeneo Ya Wazi Ambayo Wafanyabiashara Kutoka Nje Waliweka Kambi. Pia Kulikuwa Kuna Barabara Nyingi za Chini Ya Ardhi Zinazoanzia Kwenye Ngome Hii na Kufika Katika Kila Kijiji Kibosho na Nyingine Kuunganisha Machame.

– Ngome Hii Ambayo Ilikuwa Inalindwa Na Mabodigadi Ndani Na Nje Masaa 24, Iliimarisha Zaidi Utawala Wa Mangi Sina na Kuiongezea Sana Nguvu Kibosho na Hata Kumuongezea Sana Nguvu na Umaarufu Mangi Sina Mushi.

– Ngome Hii Ndio Ilikuwa Kikwazo Kwa Mangi Rindi Mandara wa Old Moshi, Kuitawala Kilimanjaro Yote Licha Ya Kukusanya Majeshi Yote Ya Karibu Kilimanjaro Nzima Pamoja na Wamasai Kwenda Kuivamia Kibosho Ili Kumkamata Mangi Sina na Kuitawala Kibosho, Ngome Hii Iliwazuia, Licha Ya Mangi Rindi Mandara na Washirika Wake Kuivamia na Kuiteka Kibosho Kwa Siku Nne. Japo, Hata Hivyo Hilo Lilipelekea Kilimanjaro Kushindwa Kuwa Moja Katika Kupambana na Wajerumani Ili Kuzuia Kutawaliwa Kikoloni.

– Ngome Hii Pia Ilipelekea Vita Ya Mwaka 1891 Kati Ya Wajerumani na Majeshi Ya Mangi Sina Kibosho Kuwa Ngumu Sana na Kuchukua Karibu Wiki Nzima, Usiku na Mchana Kumalizika.

– Ngome Hii Ilibomolewa na Wajerumani na Hata Baadhi Ya Majengo Kuchomwa Moto kwa Maagizo Ya Kapteni Johannes, Gavana wa Wajerumani Kilimanjaro Mwaka 1900. Mali ghafi Nyingi Zilizotumika Kujenga Ukuta Huu Zilichukuliwa Na Kanisa Katoliki Kibosho, Singa Kujenga Majengo Yao Ya Misheni na Nyingine Zilichukuliwa na Watu wa Kibosho kwa Matumizi Binafsi.

– Ngome Za Namna Hii Zilishajengwa Kilimanjaro Miaka Ya Zamani Zaidi Wakati wa Mangi Rongoma wa Kilema, Aliyejenga Eneo La Pofo, Kilema na Wakati wa The Great Mangi Horombo Aliyejenga Eneo La Keni, Rombo Karibu Karne Moja Nyuma Kabla Ya Hii Ya Kibosho Wakati wa Mangi Sina Mushi.

JUMBA LA KUHIFADHI SILAHA ZA KIVITA LA MANGI SINA MUSHI, KIBOSHO – MKORING’A
KIBOSHO MAUA

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

4 Comments

  1. Tafadhali ningeshauri tujaribu kuandika baadhi ya vitabu hata kimoja kuhusu utamaduni WA wachagga maana mpaka Sasa hivi tunavitafuta na hatuvipati vitabu hivyo.🙏

    1. Sawa, tutaendelea kuandika

  2. Everlyn Nicodemus says:

    Nothing

    New

    then !

    =

    In

    The

    Writings

    About

    Our

    Chaggas wa Chaggas ?

    =
    historical writings.
    =
    Past and Present ?

    The
    First
    Historian
    Of
    Chagga people
    At
    The
    Slopes
    Of
    Mountain Kilimanjaro
    Was
    Penned
    By
    A
    Chagga Historian.

    =

    Historically Documented .

    .

    Our
    =
    Chagga Tribal
    histories
    in
    writings…

    .

    .

    Remember :

    Our

    Chagga Historian!

    =

    Nathaniel Mtui !

    Aliandika

    Habari za Wachagga .

    EVERLYN

  3. Everlyn Nicodemus says:

    Kwanini ?

    Labda …

    Ukweli (…………………,)
    =
    ( freedom of speech )

    Ni ?

    =

    “ Not be punished “
    ?

    Whatever you might meant.

    Will
    I
    Get
    Published
    If
    I
    Deliver to unknown ?

    Any
    Why
    Anonymity?

    Always

    Evy

    A

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *