MACHAME NKWARUNGO, USHARIKA WA KWANZA WA KKKT, TANZANIA

KKKT – NKWARUNGO LUTHERAN PARISH, MACHAME.

Hili Ndilo Kanisa La Kwanza La Kilutheri, Afrika Mashariki.

– Wamisionari wa Kilutheri Kutoka Leipzig, Ujerumani Walifika Kilimanjaro, Mwezi Septemba Mwaka 1893 Walipokaribishwa Na Serikali Ya Wakoloni Wajerumani Kuchukua Nafasi Ya Wamisionari Waliowatangulia Kutoka London, Uingereza wa CMS Society Waliofukuzwa Kilimanjaro na Serikali Ya Wajerumani.

– Wamisionari wa CMS Society Waliokuwa Wameweka Kituo Chao Cha Misheni Eneo La Kitimbirihu, Kijiji Cha Mdawi, Old Moshi Walituhumiwa na Serikali Ya Wajerumani Kwamba Sio Wazalendo Kwa Wajerumani na Mara Nyingi Walikuwa Upande wa Wachagga Dhidi Ya Wajerumani, Hivyo Baada Ya Vita Ya Pili Kati Ya Mangi Meli na Wajerumani CMS Society Ambao Walikuwa Wameshaanza Kujiimarisha Mpaka Mashariki Ya Kilimanjaro Marangu na Mamba Walifukuzwa Kilimanjaro, Hivyo Walifungasha Virago Na Kuelekea Taveta.

– Wamisionari wa Kilutheri Walipofika Kilimanjaro Septemba, 1893 Walikichukua Kituo Hiki Cha CMS Society Cha Kitimbirihu, Old Moshi. Hata Hivyo Watu wa Old Moshi Waligoma Kuwapa Ushirikiano Kutokana na Uhasama Mkubwa Ulikuwepo Kati Yao na Wajerumani Baada Ya Kupigana Nao Vita Mbili, Vita Ya Kwanza 1892 na Vita Ya Pili 1893.

– Mwezi Oktoba, 1893 Wamisionari wa Kilutheri Waliamua Kuelekea Magharibi Ya Kilimanjaro Machame Ambapo Kulikuwa Hakujawahi Kuwa Na Dini Ya Kikristo Kabisa, Wakaelewana na Mangi Shangali na Kuanzisha Kituo Kipya Cha Misheni Ya Kilutheri Eneo La Nkwarungo, Machame.

– Nkwarungo Ikawa Ndio Makao Makuu Ya Kanisa Kwa Wakati Huu na Ndio Vituo Vingine na Makanisa Mengine Ya Kilutheri Yakaendelea Kuanzishwa Kutokea Hapo.

USHARIKA WA MACHAME, NKWARUNGO
USHARIKA WA MACHAME, NKWARUNGO
USHARIKA WA MACHAME, NKWARUNGO
USHARIKA WA MACHAME, NKWARUNGO
USHARIKA WA MACHAME, NKWARUNGO

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *