BARABARA YA RENGUA, MOSHI MJINI

RENGUA ROAD.

Hii Ni Moja Ya Barabara Katika Mitaa Ya Moshi Mjini, Lakini Ni Watu Wachache Sana Wanaoweza Kufahamu Rengua Alikuwa Ni Nani Hasa, Hii Ni Kutokana Na Sisi Wachagga Kutojihangaisha Kabisa Kufahamu Historia Yetu.

MANGI RENGUA KOMBE KIWARIA MUSHI Alikuwa Mangi Wa Machame Mpaka Mwanzoni Mwa Miaka Ya 1800. Alikuwa Mangi Mwenye Nguvu Sana Aliyetawala Nusu Ya Kilimanjaro Katika Enzi Zake, Kuanzia Magharibi Siha, Sanya Juu Mpaka Mashariki Mto Nanga Unaotenganisha Kati Ya Old Moshi Na Kirua.

Hii Barabara Inayotokea Chini Kidogo Ya Mahakamani, Inapita TRA Mkoa Kilimanjaro, Inapita Malindi, Inapita ‘Round About’ Ya Mnara Wa Saa Kisha Inateremkia Relini Huko Njoro Imepewa Jina Hili Kwa Heshima Ya Mangi Rengua Mushi.

Mangi Rengua Mushi Ni Babu Yake Mangi Ndesserua Mushi, Na Mangi Ndesserua Mushi Ni Babu Yake Mangi Abdiel Shangali Mushi.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *