BARABARA YA MANGI RINDI MOSHI MJINI

RINDI LANE STREET Ni Moja Ya Mitaa Moshi Mjini Unaoanzia Opp. Uhuru Park, Unapita St. Jose College, Kisha Kibo Tower Na Kuishia Opp. Barabara Ya Idara Ya Maji, Ni Mtaa Uliopewa Jina Hili Kwa Heshima Ya Mangi Rindi Mandara.

MANGI RINDI MANDARA MOSHI

-Alikuwa Mangi wa Old Moshi 1860 – 1891

-Ni Mangi Aliyewahi Kuwa Na Nguvu Kuliko Mangi Yeyote Kilimanjaro, Akitawala Kuanzia Uru All The Way Mpaka Usseri, Rombo Huku Akiwa Na Ushawishi Mkubwa Kilimanjaro Yote Isipokuwa Kibosho Wakati wa Mangi Sina Mushi.

-Ni Mangi Aliyeanza Kupeleka Mabalozi Nchi Za Ujerumani Na Uingereza Pamoja Na Zanzibar Kabla Ya Utawala Wa Wakoloni Afrika Huku Na Yeye Akiwa Na Wawakilishi Kutoka Serikali Hizo Katika Jumba Lake La Umangi Old Moshi, Tsudunyi.

-Ni Mangi Aliyeongoza Vita Nyingi Sana Nje Ya Kilimanjaro, Yeye Na Mangi Washirika Wake Na Vibaraka Wake Na Kuitajirisha Sana Kilimanjaro.

-Ni Mangi Aliyekuwa Anapewa Salamu Ya Heshima Sana Ya Kupigiwa Mizinga 21 Na Ujumbe Wa Wazungu Kutoka Serikali Za Ulaya Na Yeye Kuwajibu Kwa Kupiga Kombora Moja Kubwa Hewani(Canon Fire).

-Ni Mangi Aliyekuwa Anaongea Kiswahili, Kichagga, Kimasai, Kiarabu na Kwa Kiasi Kiingereza Na Kijerumani.

-Ni Mangi Aliyekuwa Na Mahusiano Mazuri Ya Kidiplomasia Na Ya Kibiashara Kwa Nchi Za Uingereza, Ujerumani, Norway, Ugiriki Na Chi Dynasty Ya China Pamoja Na Sultan Wa Zanzibar Kabla Afrika Haijaanza Kutawaliwa Na Wakoloni.

-Ni Moja Kati Ya Viongozi Wachache Sana Afrika Waliokuwa Na Umaarufu Mkubwa Sana Nchi Za Ulaya Karne Ya 19, Aliyeandikwa Sana Kwenye Vitabu Ulaya Na Kuvutia Wageni Wengi Kuitembelea Kilimanjaro Akijulikana Kama “Kilimanjaro Napoleon” au “King of the Chagga People”.

-Ni Mangi Aliyekuwa Anawasiliana Kwa Barua Na Kubadilishana Zawadi Mbalimbali Na Malkia Victoria wa Uingereza(Bibi Yake Malkia Elizabeth), Kaiser Wilhelm II Wa Ujerumani Na Mfalme wa Norway Kabla Ya Wakoloni Kutawala Africa.

-Ndiye Mangi Aliyesababisha Leo Hii Moshi Mjini Na Eneo Lote La Moshi Linaitwa Moshi.

-Ni Mangi wa Kwanza Kupambania Kujenga Shule Rasmi(Formal Schooling) Kilimanjaro Kuanzia Miaka Ya 1870’s.

-Pia Ndiye Baba Yake Mangi Meli Mandara Aliyewashinda Vita Wajerumani Na Kuwafukuza Kabisa Kilimanjaro Kwa Zaidi Ya Mwaka Mmoja. -N.k, n.k.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *