UKOO WA TEMBA.

– Ukoo wa Temba ni ukoo mkubwa sana maarufu na mashuhuri unaopatikana kwa wingi zaidi katikati na katikati magharibi ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo wa wenye watu wengi sana wanaofanya kazi maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Temba kwa uchaggani unasemekana kwamba ulikuwa na makazi ya mwanzoni na ya kudumu katika maeneo ya kijiji cha Mmbahe katika ukanda wa juu wa Marangu au maeneo ya jirani. Lakini baadaye wakati ukoo wa Mtui wa nchi ya Mshiri, Marangu wanatanua himaya yao wakati wa utawala wa Mmori mjukuu wa Kilaweso walijaribu kuwalazimisha Teemba na watu wake kukaa chini ya utawala wao, hili pengine lilitokea kwenye karne ya 16 au 17.

– Hata hivyo wajumbe waliotumwa kupeleka taarifa hizi kwenye himaya ya Temba ambao walikuwa wanajaribu kuwaonyesha kwamba ukoo wa Mtui ni wenye nguvu sana na hivyo wameamua kutawala eneo lote la ukanda wa juu wa Marangu waliishia kuuawa na mmoja pekee ndio aliachwa hai na kuruhusiwa kurudi Mshiri kupeleka tangazo la vita. Kitendo hicho kilimkasirisha sana Mmori mtawala wa Mshiri pamoja na baraza lake hivyo walikusanya majeshi yao na kuvamia ngome ya Temba na watu wake.

– Watu wa ukoo wa Temba walishtukizwa na vita kubwa ikapiganwa ambapo walizidiwa na kushindwa na hivyo kutawanyika na kukimbia. Wachache walikimbilia upande wa magharibi na kuweka makazi maeneo ya Mamba na Mwika. Lakini wengi zaidi wakiongozwa na kiongozi mkuu wa ukoo walikimbilia upande wa mashariki ambapo walikimbizwa sana kupitia Kilema, Kirua Vunjo na Old Moshi mpaka kuvuka mto Rau na kuweka makazi ya kudumu katika eneo la himaya ya umangi Uru.

– Waliweka utawala wao katika eneo la Uru lakini baada ya kuishi kwa muda mrefu walikutana na changamoto nyingine kubwa. Ukoo mmoja wa watu matajiri wa mifugo wenye asili ya kimasai walioongozwa na Mzee wa ukoo aliyeitwa Mkoruo walishirikiana na koo nyingine za maeneo hayo kupambana ukoo wa Temba ili kufanikiwa kutawala eneo hilo. Ukoo huu wa Mzee Mkoruo kwa kuwa walikuwa na mali nyingi waliweza kupata kuungwa mkono na marafiki wengi waliowategemea na kufanikiwa kuusambaratisha tena ukoo wa Temba.

– Watu wengi wa ukoo huu walikimbia tena kuelekea magharibi huko Kibosho na wengine mashariki huko Old Moshi na wengine zaidi kusambaa katika maeneo mbalimbali ya eneo la himaya ya umangi Uru. Hivyo ukoo wa Temba uliendelea kukua na kuimarika ukiwa na watu wengi waliosambaa mpaka magharibi kabisa lakini wengi wakiwa ni machachari na wenye kujituma sana kimaisha.

– Hivyo ukoo wa Temba umesambaa na unapatikana kuanzia maeneo ya Shari/Uraa, Machame.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Manushi, Kibosho.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sambarai, Kibosho.

– Ukoo wa Temba unapatikana katika kata ya Kindi, Kibosho.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uri, Kibosho.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uchau Kaskazini, Kibosho.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kirima Kati au Kidachini Kibosho.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Boro, Kibosho.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Okaseni na Mrawi, Uru.

– Ukoo wa Temba unapatikanakwa wingi sana Uru, Mawela na eneo la Kimanganuni.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Njari, Uru.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Shimbwe, Uru.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mnini, Uru.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kyaseni, Uru.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kishumundu, Uru.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Materuni na Mruwia, Uru.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mwasi Kaskazini na Mwasi Kusini, Uru.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Tela, Old Moshi.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kmare, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mmbahe, Marangu.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Komela, Marangu.

– Ukoo wa Temba unapatikana kwa kiasi katika eneo la Mamba.

– Ukoo wa Teemba unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

-Ukoo wa Temba unapatikana kwa kiasi pia baadhi ya maeneo ya vijiji vya Rombo.

Kwa sababu ukoo wa Temba ni ukoo mkongwe na mashuhuri sana bado kuna taarifa nyingi ambazo hazijulikani kuhusu ukoo huu, tunaomba mchango wa mawazo juu ya mengi tusiyoyafahamu kuhusu ukoo wa Temba ili kuweza kuongezea kwenye tafiti na kuwa na maudhui zaidi kwa faida ya jamii yetu kwa ujumla. Tunahitaji mchango wako zaidi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Temba?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Temba?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Temba?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Temba una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Temba wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Temba kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Temba?

7. Wanawake wa ukoo wa Temba huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Temba?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Temba?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *