UKOO WA OLOMI/ULOMI.

– Olomi/Ulomi ni ukoo mkubwa kiasi wa wachagga wanaopatikana kwa wingi upande wa magharibi na magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro na kwa kiasi katikati ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi waliosambaa maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Chimbuko halisi la ukoo wa Olomi/Ulomi bado haijawa rahisi kulipata lakini ukoo huu unapatikana kwa wingi kwa baadhi ya maeneo ya vijiji na kwa uchache kwenye vijiji vingine. Baadhi ya wachagga wa kutokea kwenye ukoo wa Olomi/Ulomi ni watu wenye vipaji mbalimbali na wanafanya vizuri sana kwenye nyanja mbalimbali za kimaisha hususan katika ujasiriamali, biashara na taaluma. Moja kati ya wafanyabiashara wakubwa kutoka kwenye ukoo huu anayefahamika sana ni Mr. Patrick Ngiloi Ulomi maarufu kama Panone mwenye makampuni mbalimbali Moshi, Arusha na Dar es Salaam.

– Ukoo wa Olomi/Ulomi uliendelea kusambaa kwa karne kadhaa zilizopita na unapatikana kwa wingi na kwa uchache kwa baadhi ya vijiji upande wa magharibi ya mbali, magharibi ya kati na katikati ya eneo la Uchagga, Kilimanjaro.

– Hivyo ukoo wa Ulomi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Lukani, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mashua, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mbosho, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mroma, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Lemira Kati, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Isuki, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mbweera, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mboreny, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ngira, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mudio, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kware, Masama.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Uswaa-Mamba, Machame.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Uswaa, Machame.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Nkuu, Machame.

– Ukoo wa Ulomi unapatikana kwa uchache katika kitongoji cha Kimbushi, Machame.

– Ukoo wa Olomi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Manushi Ndoo, Kibosho.

– Ukoo wa Olomi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Umbwe Sinde, Kibosho.

– Ukoo wa Olomi unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kifuni, Kibosho.

– Ukoo wa Olomi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Umbwe Onana, Kibosho.

– Ukoo wa Olomi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Umbwe Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Olomi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.

– Ukoo wa Olomi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Dakau, Kibosho.

– Ukoo wa Olomi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Boro, Kibosho.

– Ukoo wa Olomi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

Karibu kwa mchango zaidi wa mawazo kuhusiana na ukoo wa Olomi/Ulomi ulioenea zaidi upande wa magharibi ya mbali na magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro na kwa kiasi maeneo ya katikati. Tunajitaji msaada wa kusaidia kupatikana maudhui zaidi yatakayoongeza katika maktaba ya ukoo wa Olomi/Ulomi ili kuweza kujenga kizazi bora kinachojitambua ili kurahisisha katika kujenga shauku ya kule tunakoelekea.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Olomi/Ulomi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Olomi/Ulomi?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Olomi/Ulomi?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Olomi/Ulomi?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Olomi/Ulomi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Olomi/Ulomi wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Olomi/Ulomi kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Olomi/Ulomi?

9. Wanawake wa ukoo wa Olomi/Ulomi huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Olomi/Ulomi?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Olomi/Ulomi?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Olomi/Ulomi?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Olomi/Ulomi kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *