UKOO WA CHAMI

– Chami ni ukoo mkubwa wa wachagga wanaopatikana upande wa magharibi ya kati kuelekea magharibi zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Chami ni kati ya koo ambazo kihistoria ziliweza kutoa watu hodari na mashuhuri katika utaalamu wa ufinyanzi na wafanyabiashara wa bidhaa za ufinyanzi hususan vyombo vya nyumbani.

– Vyombo vingi vya nyumbani vilivyotengenezwa na wachagga wa ukoo wa Chami na koo nyingine zilizokuwa zinatengeneza bidhaa za ufinyanzi zilipendwa zaidi Uchaggani kuliko vile vilivyokuwa vinanunuliwa kutoka nje ya Uchagga, Kilimanjaro kama vile Upare na kwengineko.

– Ukoo wa Chami uliendelea kukua na kusambaa zaidi maeneo ya vijiji vya magharibi ya kati ya Uchagga kuelekea magharibi zaidi kwa baadhi ya vijiji wakipatikana kwa uchache na kwingine wakipatikana kwa wingi zaidi.

– Hivyo ukoo wa Chami unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Usari, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tella, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mulama, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa wingi sana sana katika kijii cha Orori, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kombo, Kibosho.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Umbwe Sinde, Kibosho.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Umbwe Onana, Kibosho.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Umbwe Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kifuni, Kibosho.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kindi Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kindi Muyuni, Kibosho.

– Ukoo wa Chami unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Sungu, Kibosho.

Tunahitaji kufahamu zaidi kuhusiana na ukoo wa Chami na namna ulivyosambaa upande wa magharibi wa Uchagga, tunaomba mchango wako wa mawazo ili kuongeza maarifa zaidi na maudhui yatakayoendelea kusomwa na watu zaidi na hata kizazi kinachokuja. Maudhui yatakayoongezeka kwenye maktaba ya ukoo wa Chami na wachagga wa ujumla ni sehemu muhimu ya ukoo huu na wachagga kwa ujumla kupiga hatua kuelekea katika ngazi za juu zaidi za kujitambua na kujenga kujitambua na kujiamini.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Chami.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Chami?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Chami?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Chami?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Chami una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Chami wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Chami kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Chami?

9. Wanawake wa ukoo wa Chami huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Chami?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Chami?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Chami?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Chami kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *