UKOO WA MASSAM.

– Massam ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi sana maeneo ya katikati au mashariki ya karibu ya Uchagga na maeneo ya mwishoni mwa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Massam ni ukoo wa watu jasiri sana na wanaofanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi kitaaluma na hata katika ujasiriamali.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Massamu ulikuwa unatoa wanajeshi hodari na walinzi katika utawala wa Mangi. Moja kati ya wanajeshi maarufu katika utawala wa Mangi Meli Old Moshi alitokea ukoo wa Massamu. Kwa Old Moshi ukoo huu wa Massamu kuna eneo ana mtaa kabisa unaoitwa Masamuni kwa kuwa wanapatikana kwa wingi zaidi eneo hilo.

– Hata hivyo ukoo wa Massam umesambaa na unapatikana kwa wingi na kwa uchache kwenye vijiji mbalimbali tofauti.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Msaranga, Old Moshi.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimangarao, Mwika.

– Ukoo wa Massam unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

Karibu kwa taarifa zaidi kuhusiana na ukoo wa Massam ambao umesambaa katika vijiji mbalimbali na wenye historia ya aina yake lakini ukiwa na taarifa chache sana kuuhusu. Tunahitaji kuongeza maudhui zaidi kwenye maktaba ya ukoo wa Massam ili kuendelea kujenga uelewa mpana na kujitambua sana miongoni mwa wachagga. Hili linaweza kusaidia katika kutujengea hamasa zaidi na mshikamano sambamba na ari ya kuongeza bidii kubwa katika maisha katika nyanja zote katika kuyaendea mafanikio makubwa.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Massam.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Massamu?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Massam?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Massam?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Massam una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Massam wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Massam kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Massam?

9. Wanawake wa ukoo wa Massam huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Massam?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Massam?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Massam?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Massam kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 717 452 790.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *