VYAMA VYA SIASA VYA WACHAGGA – KILIMANJARO

VYAMA VYA SIASA VYA WACHAGGA.

1. Kilimanjaro Chagga Citizens Union (KCCU).

2. Chagga Democratic Pary (CDP).

Wachagga Walipata Kuwa na Vyama Viwili Vikubwa Vya Kisiasa Ambavyo Vyote Vilipambana Kufikia Kuwa na Taifa Huru La Wachagga Wakati Harakati Za Utaifa Rasmi Zikiendelea Kupamba Moto, Kilimanjaro Kuanzia Miaka Ya 1920’s.

Chama Cha Kilimanjaro Chagga Citizens Union (KCCU) Ndio Chama Cha Siasa Cha Mwanzo Zaidi Kuanzishwa Kilimanjaro Kilichoasisiwa na Wanaharakati wa Uchagga Wakina Joseph Merinyo Maro, Petro Njau na Wenzao Kupigania Maslahi Ya Kisiasa Ya Taifa Huru La Wachagga.

Chama Cha KCCU Katika Kampeni Za Kuchagua Mangi Mkuu wa Wachagga Ndicho Kilimpigania Kwa Nguvu Zote Mangi Thomas Lenana Marealle Mjukuu wa Mangi Ndegoruo Marealle Ambaye Hakuwa na Uzoefu Binafsi wa Siasa za Uchaggani na Hakuwa Chaguo La Waingereza, Lakini Akafanikiwa Kushinda Umangi Mkuu Katika Uchaguzi Uliokuwa na Ushindani Mkali Uliohusisha Wagombea Wanne. Lengo La KCCU Lilikuwa Kupigania Maslahi Ya Taifa Huru La Wachagga Dhidi Ya Waingereza. Baadaye Miaka Ya 1950’s Kilianzishwa Chama Kingine Cha Kisiasa Kilichoitwa Chagga Democratic Party (CDP) Kilichoasisiwa na Wakina Solomon Eliufoo Ambacho Kilipigania Mabadiliko Ya Kikatiba Ya Serikali Ya Wachagga Iliyokuwa Inaongozwa Na Mangi Mkuu, Mwishoni Mwa Miaka Ya 1950’s.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. In vyema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *