KAMBI YA WATALII “HOROMBO HUT” MARANGU ROUTE, MLIMA KILIMANJARO

HOROMBO HUT!

Hii Ni Kambi Ya Pili Ambayo Watalii Wanaopanda Mlima Kilimanjaro Kupitia Njia Ya Marangu(Marangu Route) Wanalala Siku Ya Pili Ya Kupanda Mlima. Kambi Hii Imepewa Jina Hili Kwa Heshima Ya Mangi Horombo.

MANGI HOROMBO

-Alikuwa Mangi wa Keni, Rombo Mpaka Mwanzoni Mwa Miaka Ya 1800.

-Alitawala Zaidi Ya Nusu Ya Kilimanjaro, Kuanzia Katikati Kuelekea Mashariki Katika Nyakati Zake Kuanzia Eneo La Kirua, Kilema, Marangu, Mamba, Mwika Na Rombo Yote Mpaka Usseri, Yaani Vunjo na Rombo Yote Ilikuwa Chini Ya Utawala Wake.

-Ni Moja Kati Ya Wamangi Waliojenga Ngome Kubwa Na Imara Sana Kilimanjaro, Aliyoijenga Katika Eneo La Keni, Rombo.

-Alikuwa Na Wataalamu Wa Kila Aina Kuimarisha Himaya Yake Chini Ya Utawala Wake Kuanzia Kirua Vunjo Mpaka Usseri, Rombo Kuanzia Wanajeshi, Mainjinia, Wakulima, Wawindaji N.k.,

-Inasemekana Akiwa Bado Kijana Aliwahi Kuua Tembo Peke Yake.

-Alikuwa Mangi Hodari Sana Kwenye Vita Ambapo Yeye Mwenyewe Alikuwa Anaenda Vitani Sambamba Na Jeshi Lake Na Kuingia Kwenye Mapambano Kiasi Cha Kuogopwa Sana Na Himaya Zote Za Jirani Na Kilimanjaro, Na Aliogopwa Zaidi Na Wamasai Ambao Wanasemakana Walikuwa Ni Wavamizi Wakubwa Wa Maeneo Mengi.

-Mangi Horombo Pia Ndiye Babu Yake Mangi Tengia Wa Keni, Mangi Tengia Ambaye Mangi Ndegoruo Marealle wa Marangu Alioa Binti Yake Aliyeitwa Makyaleni Na Kumzaa Mangi Petro Itosi Marealle Aliyekuja Kuwa Mangi Mwitori Wa Jimbo La Vunjo, Uchagga 1946 Na Kutuandikia Kitabu Cha “Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani Na Ahera”.

-Historia Inamtambua Mangi Horombo Kuwa Ni Moja Kati Ya Wamangi Bora Zaidi Kuwahi Kutokea Kilimanjaro.

-Eneo Lote La Rombo Ambalo Kwa Sasa Ni Wilaya Nzima Ya Rombo Limeitwa Kwa Heshima Ya Jina Lake.

Jina Rombo Ni Utamkaji wa Kiingereza Na Kiswahili, Kwa Kichagga Huitwa Horombo Kama Lilivyo Jina La Mangi Horombo Mwenyewe.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *