– Kiria ni ukoo wa wachagga wanaopatikana zaidi maeneo ya upande wa magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wa watu wanaojulikana kuwa wajasiri sana na wenye historia ya kutoa wanajeshi hodari sana wakati wa tawala za wamangi zamani. Ukoo wa Kiria ni ukoo wenye watu wanaofanya vizuri sana katika biashara na ujasiriamali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi na baadhi wana mafanikio makubwa.
– Ukoo wa Kiria ulikuwa ni ukoo mashuhuri ndani ya himaya ya umangi iliyojulikana kama himaya ya Kindi kabla ya baadaye kuja kuunganishwa na kuwa sehemu ya himaya ya umangi Kibosho.
– Kutoka kwenye historia ukoo wa Kiria unasemekana kuwa ulitokea maeneo ya Vunjo, Uchagga, Kilimanjaro na kuelekea mashariki na kuweka makazi yao katika eneo la iliyokuwa himaya ya umangi Kindi. Ukoo wa Kiria unatambulika pia kwamba ulikuwa ni moja ya zile koo za wachagga wafua vyuma ambao walijihusisha na shughuli za uhunzi na kufua vyuma hivyo kutengeneza silaha bora sana za kivita.
– Himaya ya umangi Kindi ilijulikana zamani kwa uhodari na ujasiri sana vitani na kuna nyakati iliweza kujisimamia ikizikabili himaya mbili kubwa zenye nguvu Kilimanjaro ambazo ni himaya ya umangi Machame kwa upande wake wa magharibi na himaya ya umangi Kibosho kwa upande wake wa mashariki. Himaya ya umangi Kindi ambapo ukoo huu wa Kiria ulikuwa na mchango mkubwa katika kuiimarisha kisilaha na kijeshi iliweza kujenga watu imara na jasiri sana ambao mpaka leo uthubutu wao unaweza kuonekana.
– Lakini pia kuna tafiti nyingine za kihistoria ambazo zinauhusisha ukoo wa Kiria kuwa ni ndugu wa damu na koo nyingine mashuhuri za kufua vyuma Uchaggani, Kilimanjaro za Makundi na Malisa. Kuna baadhi taarifa zinadai kwamba ukoo wa Kiria, Makundi na Malisa wana undugu wa damu na walikuwa ni watu wenye kuheshimika sana kwa shughuli za ufuaji vyuma ambazo zilikuwa ni muhimu sana katika kuimarisha himaya za zamani kijeshi pamoja na kuboresha maeneo mengine kwa kutumia teknolojia hiyo ya vifaa vya chuma.
– Ukoo wa Kiria umeendelea kusambaa maeneo ya vijiji zaidi vya maeneo ya magharibi ya kati ya Kilimanjaro na unapatikana kwa vijiji vingi zaidi nje ya iliyokuwa himaya ya umangi Kindi.
– Hivyo ukoo wa Kiria unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Manushi Sinde, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Manushi Ndoo, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Umbwe Sinde, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkomongo, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Umbwe Onana, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kindi Juu, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kindi Kati, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sambarai, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kindi Muyuni, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kindi Msasani, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mloe, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkomilo, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Dakau, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Otaruni, Kibosho.
– Ukoo wa Kiria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mweka, Kibosho.
Kutokana na taarifa nyingi muhimu juu ya iliyokuwa himaya ya umangi Kindi kupotea na hata taarifa nyingi sahihi juu ya historia ya ukoo wa Kiria kupotea tunahitaji kupata taarifa zaidi kutoka kwenye chanzo chochote juu ya ukoo wa Kiria. Taarifa hizi zitasaidia kuongeza maudhui ya ukoo huu wa Kiria ambayo yanaweza kujenga hamasa na hata mshikamano baina ya wanaukoo na wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kutengeneza maudhui zaidi na kuongeza sana kwenye maktaba ya koo za wachagga na jamii ya wachagga kwa ujumla ili kujenga uelewa sahihi na kuhimiza na kuhamasisha maendeleo zaidi kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja, ngazi ya ukoo na jamii ya wachagga kwa ujumla. Karibuni sana.
Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kiria.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kiria?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kiria?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kiria?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kiria una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Kiria wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kiria kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kiria?
9. Wanawake wa ukoo wa Kiria huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kiria?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kiria?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kiria?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kiria kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
Whatsapp +255 754 584 270.