UKOO WA MASSAO.

– Massao ni ukoo maarufu wa wachagga unaopatikana zaidi maeneo ya ukanda wa magharibi ya karibu na katikati ya Uchagga, Kilimanjaro. Kutoka kwenye simulizi za watu wanaufananisha ukoo huu kama ukoo uliotokana na ukoo wa Massawe kwa kiasi ambacho umekaribia kufanana majina yake japo wenye unapatikana maeneo machache sana ukilinganisha na ukoo wa Massawe. – …

UKOO WA FOYA.

– Foya ni ukoo wa wachagga wanaopatikana zaidi katika eneo la katikati au magharibi ya kati ya nchi ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu makini sana ambapo katika miaka ya zamani sana ulikuwa ni moja kati ya koo mashuhuri zilizotoa mainjinia wataalamu wa miundombinu za umwagiliaji na mifereji ya maji kwa ujumla. Hata …

UKOO WA KINABO.

– Kinabo ni ukoo mashuhuri wa wachagga unaotokana na watawala waliowahi kupita zamani na kupata umaarufu au umashuhuri katika himaya husika. Ukoo huu unapatikana kwa kiasi maeneo ya Lyamrakana, Marangu na kwa wingi kiasi maeneo ya Mkuu, Rombo. Huu kwa sehemu kubwa ni ukoo wa watu makini na wasomi zaidi ambao wanafahamiana kwa karibu na …