Mfahamu ELIFURAHA NDESAMBURO URIO MAREALLE.

– Elifuraha alizaliwa huko Mwika, Moshi, Kilimanjaro mwaka 1929. – Alisoma katika shule ya Sekondari ya wasichana Ashira ambapo baadaye alikuja pia kufundisha tena kama mwalimu katika shule hiyo. – Mwaka 1955 Elifuraha alikuwa mmoja kati ya wanawake watatu wa kwanza kuwa wabunge Tanganyika, yeye peke yake akiwa ndiye mwafrika. Hivyo ni mwanamke wa kwanza …