UKOO WA MREMI.

– Mremi ni ukoo wa wachagga wenye umaarufu kiasi unaopatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa mwishoni mwa mashariki ya kati ya Uchagga na mwanzoni mwa ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Ni ukoo wenye watu mbalimbali makini wanaofanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali hasa biashara na ujasiriamali.

– Kutoka kwenye historia Mremi ina asili ya eneo la mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro hususan katika himaya ya umangi Kilema na Marangu. Katika historia kwenye kitabu chetu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” tunaona kwamba Mremi na ndugu yake mdogo aliyeitwa Lyimo walikuwa ni watoto wa Wamba ambaye ni mtoto wa Temi na mjukuu wa Mlambaki. Kwa bahati mbaya Mremi ambaye alikuwa ni mtoto mkubwa wa kiume hakuwa hodari sana katika vita na mapambano na maisha kwa ujumla kwa hiyo hakupendwa sana na wazazi na matokeo yake nafasi akapewa mdogo wake aliyeitwa Lyimo ambaye alikuwa jasiri, imara na mpambanaji hivyo Mremi aliondoka na kwenda kuanzisha ukoo mwingine ulioitwa Makite.

– Lakini baadaye tena tunaona kutoka kwenye kitabu chetu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” katika himaya za umangi Marangu na Kilema kwamba Mremi na ndugu yake mdogo aliyeitwa Riwa walikuwa ni watoto wa Ngowi ambaye alikuwa ni Mangi wa himaya ya umangi Marangu. Kisha Marangu ilipovamiwa mwishoni mwa miaka ya 1600 na wavamizi kutokea upande wa mashariki Mremi na baba yake Ngowi walikimbilia Kilema na kumwacha mdogo wake Mremi hapo Marangu ambaye aliamua kukusanya majeshi akisaidia na majenerali wajasiri wakapambana na wavamizi hao na kuwashinda na kufanikiwa kuiokoa himaya ya Marangu dhidi ya wavamizi hao.

– Ngowi alipokimbilia Kilema kutokana na utajiri mkubwa aliokuwa nao ambao alikuwa ameujenga Marangu alifanikiwa kuwa ushawishi mkubwa. Na kwa kutumia utajiri huo alijenga ushawishi zaidi na kukubalika Kilema kiasi cha kuweza kukalia kiti cha utawala Kilema japo sio Kilema yote kwa wakati huo. Koo zilizokuwa na nguvu kama ukoo wa Mosha waligoma kumtambua na hivyo Kilema kuwa katika migawanyiko. Baada ya Ngowi kutawala kwa muda Kilema alimtawalisha mtoto wake huyo mkubwa wa kiume aliyeitwa Mremi sasa. Mangi Mremi akaendelea kuwa Mangi wa Kilema huku akijenga ushawishi mkubwa zaidi na baadaye kupata msaada wa kijeshi kutokea Mamba na kuitawala Kilema yote. Kwenye kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” tunaona kwamba baadaye Mremi alimtawalisha mtoto wake aliyeitwa Nyange mwanzoni au katikati ya miaka ya 1700 kuwa Mangi wa Kilema.

– Hivyo jina Mremi au ukoo wa Mremi una vyanzo mbalimbali tata vya namna ulivyokuja kuwa na kutanuka. Hata hivyo kwa sasa tunaona ukoo huu umeenea zaidi upande wa mashariki zaidi ya eneo ambao ulionekana zaidi zamani. Ukoo wa Mremi umeenea na unapatikana katika vijiji zaidi.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Matala, Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Uuwo, Mwika.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa uchache katika kitongoji cha Kirimeni, Mrimbo Uuwo, Mwika.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Lole, Mwika.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Manda Juu, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Aleni Chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Mremi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Shimbi Kati, Shimbi, Mkuu, Rombo.

Ukoo wa Mremi ni ukoo wenye historia kubwa ya nyuma lakini yenye utata zaidi juu ya namna vizazi vyake vilivyokwenda na kuishia kuwa. Hivyo tunahitaji kupata maudhui zaidi ya ukoo wa Mremi ili kuweka katika maktaba ya ukoo huu sambamba na maktaba ya wachagga kwa ujumla ili kuweza kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Lengo la kukusanya maudhui haya ni kuweza kujenga hamasa, umoja na mshikamano kwa kizazi kinachokuwa katika kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja, ukoo na jamii nzima ya wachagga.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Mremi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mremi?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mremi?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mremi?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mremi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mremi wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mremi kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mremi?

9. Wanawake wa ukoo wa Mremi huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mremi?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mremi?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mremi?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mremi kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

    1. Ahsante sana Belinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *