Mfahamu ELIFURAHA NDESAMBURO URIO MAREALLE.

– Elifuraha alizaliwa huko Mwika, Moshi, Kilimanjaro mwaka 1929.

– Alisoma katika shule ya Sekondari ya wasichana Ashira ambapo baadaye alikuja pia kufundisha tena kama mwalimu katika shule hiyo.

Mwaka 1955 Elifuraha alikuwa mmoja kati ya wanawake watatu wa kwanza kuwa wabunge Tanganyika, yeye peke yake akiwa ndiye mwafrika. Hivyo ni mwanamke wa kwanza mweusi kuwa mbunge ndani ya bunge la Tanganyika katika kipindi cha utawala wa waingereza.

– Mwaka 1948 alifunga ndoa na Thomas Marealle ambaye miaka 3 baadaye alikuja kuwa Mangi Mkuu wa wachagga.

– Mwaka 1952 baada ya Mangi Mkuu wa wachagga kuhutubia taifa la wachagga naye alitoa hotuba fupi na kisha kutangazwa rasmi kama mama wa taifa la wachagga.

– Elifuraha Marealle alifariki mwezi Oktoba, mwaka 2015 na kuzikwa nyumbani kwake huko Lyamrakana, Marangu sambamba na Mangi Mkuu wa wachagga Thomas Marealle.

Karibu kwa Maoni au Mchango zaidi kuhusu Mkamanga Elifuraha Ndesamburo Urio Marealle.

Karibu sana.

Urithi Wetu Wachagga.

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. Hello,
    Naomba ufafanuzi. Jina lake naona lina majina matatu ya ukoo; Ndesamburo, Urio na Marealle. Hili la mwisho najua ni la mume wake. Hayo mawili? Lingekua moja ningefikiri kuwa ni la ukoo alikozaliwa.

    1. Ndesamburo sio jina la ukoo, Ndesamburo ni jina la babu. Urio ndio jina lake la ukoo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *