UKOO WA NATAI

– Ukoo wa Natai ni ukoo mkongwe pia na mashuhuri sana upande wa Magharibi ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo ambao unapatikana kwa wingi zaidi katika eneo la Masama magharibi katika vijiji vya Lukani, Mashua, Nkwansira, Ng’uni, Kyuu, Losaa n.k. Ukoo wa Natai wanapatikana kwa wingi pia katika vijiji vya himaya ya umangi Sanya Juu. – …

UKOO WA MASAKI.

– Ukoo wa Masaki ni ukoo maarufu katika eneo la himaya ya umangi Siha/Sanya Juu katika vijiji vya Samaki Maini na Mae. Wachagga wa ukoo wa Masaki wakiwa wameshuka kutoka kwenye plango ya Shira waliweka makazi yao ya mwanzoni ya kudumu katika kijiji cha Samaki Maini sambamba na ukoo wa Orio/Urio na Kileo. – Kutoka …

UISLAMU UCHAGGANI.

– Kupitia historia tunafahamu kwamba wachagga wa kwanza kuoandoka kwenye dini asili ya wachagga na kujiunga na dini za kigeni ilikuwa ni katika muongo wa mwisho wa karne ya 19. Hii ilikuwa ni mwaka 1892 wamisionari wa misheni ya kianglikana ya CMS ilipowabatiza wachagga wawili katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi mwezi Julai 1892 kwa …