TUENZI, TUJIVUNIE NA KUHIFADHI VYETU. – WACHAGGA

Tusikilize na Kutangaza Nyimbo Zetu, Siku Zote Wimbo Hupendwa Baada Ya Kuusikiliza Mara Kadhaa. Wimbo Huwa Maarufu Kwa Kupigwa Mara Kwa Mara Na Kupendwa Na Watu Wengi.

Wasanii Wetu Kadhaa Wa Kichagga Wanaokuja Kwa Kasi Na Kufanya Vizuri, Tuwape Nafasi Zaidi Ili Wakue Maana Wana Mambo Mengi Sana Ya Kuimba, Wanahitaji Kuimba Maelfu Ya Nyimbo Zinazohifadhi Tamaduni Zetu Na Jumbe Mbalimbali Zinazohusu Asili Yetu.

Lugha Yetu Inahifadhiwa Na Kutangazwa Zaidi Kupitia Hizi Nyimbo. Ndio Lugha Pekee Tunayoweza Kujivunia Duniani Inayotoka Kwenye Asili Yetu, Lugha Tuliyorithi Kutoka Kwa Babu Zetu(Ubunifu Wetu Wa Vizazi Na Vizazi Vyetu). Huwezi Kujivunia Kiingereza, Kiingereza Wanajivunia Waingereza, Kijerumani Wanajivunia Wajerumani. Kiswahili Ni “Lingua Franca”, Hakuna Jamii Inayojivunia “Lingua Franca” Duniani, Lugha Unayoweza Kujivunia Wewe Ni Kichagga Na Moja Ya Njia Za Kuenzi Na Kutangaza Kichagga Ni Kupitia Nyimbo. Tusikilize Nyimbo Zetu Kama Kweli Tunajiheshimu Na Kuheshimu Tamaduni Zetu Na Kama Kweli Tunahitaji Lugha Yetu Idumu Kwa Maelfu Ya Miaka. Wenzetu Kenya Na Afrika Kusini Wameingiza Kwenye Mitaala Na Wameanza Kuzisoma Shule, Tumebaki Sisi Tu.

Kama Tunaweza Kuwaunga Mkono Makhirikhiri Kutoka Botswana Ambao Hata Hatuelewi Lugha Yao, Na Wasanii Wengine Wengi Ambao Wanaburudisha Lakini Hawaongezi Chochote Kwenye Asili Yetu Naamini Tunaweza Kuwaunga Mkono Hawa Wasanii Wetu Wanaoendelea Kuhifadhi Na Kutangaza Asili Yetu Wakawa Maarufu Zaidi Na Hata Kunufaika Zaidi Ili Wapate Ari Ya Kuendelea Kufanya Vizuri.

Lugha Ya Kichagga Haipaswi Kufa, Itaendelea Kudumu Na Kuwa Bora Zaidi Na Zaidi Na Watoto Wetu Kuienzi Na Kujivunia.

“AIKA MAE” – LYIMO

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. Tunashukuru kwa kazi kubwa mnayoendelea nayo ya kuhifadhi urithi wetu wa kiChagga. Nimefarijika kuona kazi nyingi nzuri zinazoendelea kufanyika.
    Nimefanya utafiti mdogo wa kuona namna nyimbo zetu za kitamaduni zinaweza kutumika kama makavazi ya elimu ya kitamaduni ya mwaAfrika.
    https://drive.google.com/file/d/1FKkxaHIlQo_pdYcfn7883gVH0TztZvxn/view?usp=drivesdkhttps://drive.google.com/file/d/1FKkxaHIlQo_pdYcfn7883gVH0TztZvxn/view?usp=drivesdk

    1. Ahsante sana. Karibu sana Kavishe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *